Machapisho

Ajira za walimu na afya tamisemi june 2022

 TAARIFA KWA UMMA KUHUSU AJIRA MPYA ZA UALIMU 
NA KADA ZA AFYA

1. UTANGULIZI

Ndugu Wanahabari;

Mtakumbuka kuwa mwezi Aprili, 2022; Rais wa Jamhuri ya

Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, alitoa

kibali cha ajira kwa kada za Ualimu na Afya, kwa ajili ya kuajiri 

walimu 9,800 wa Shule za Msingi na Sekondari, na wataalam 

wa Afya 7,612.

Baada ya kupata kibali cha ajira, Ofisi ya Rais – TAMISEMI ilitoa 

tangazo kwa wahitimu mbalimbali wa Ualimu na Kada za Afya,

kuwasilisha maombi ya kazi, kupitia mfumo wa kielektroniki wa 

kupokea na kuchakata maombi ya ajira, kuanzia tarehe 

20/04/2022 hadi 08/05/2022. Jumla ya maombi 165,948

yakiwemo ya Wanawake 70,780 na Wanaume 95,168

yaliyopokelewa kwenye mfumo, ambapo maombi ya Kada za Afya 

ni 42,558, na Kada ya Ualimu ni 123,390.

Ndugu Wanahabari;

Ili kufanikisha mchakato wa ajira, Ofisi ya Rais – TAMISEMI 

iliunda Timu Maalum, ya kufanya Uchambuzi wa Maombi ya 

Ajira, iliyohusisha Taasisi mbalimbali. Taasisi hizo ni pamoja na 

Ofisi ya Rais Ikulu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa 

Umma na Utawala Bora, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Ofisi ya 

Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Wizara 

ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania 

(TCU), Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Ufundi Stadi (NACTVET), Sekretarieti ya 

Ajira, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa

(TAKUKURU), na Mabaraza ya Kitaalamu katika Sekta ya Afya.

(a)Vigezo Vilivyotumika

Ndugu Wanahabari;

Kutokana na idadi ya waombaji kuwa kubwa, Timu ya 

Uchambuzi wa Maombi ya Ajira ilipewa vigezo vilivyoandaliwa 

kama mwongozo wa kutoa ajira kwa waombaji, kwa lengo la 

kuhakikisha uwepo wa haki na uwazi katika zoezi hili. Katika 

kuhakikisha usawa wa kijinsia unafikiwa, katika vigezo 

vilivyotumika kupata waajiriwa wapya kwa mwaka 2022, kila 

kigezo kilizingatia uwiano wa kijinsia. Vigezo vilivyotumika ni 

kama ifuatavyo: -

i. Mwaka wa kuhitimu

Katika kigezo hiki, kipaumbele kimetolewa kwa waombaji wenye 

sifa waliotangulia kuhitimu kwa mfuatano wa mwaka, kulingana 

na hitaji la kada/kozi au kiwango cha Elimu, na pia mwaka wa 

kozi ilivyoanza kutoa wahitimu.

ii. Umri wa kuzaliwa

Waombaji wenye sifa waliopangwa kwa mujibu kigezo namba (i) 

hapo juu walipangwa kulingana na umri wa kuzaliwa. Lengo ni 

kuwawezesha waombaji wenye umri unaokaribia miaka 45 

kuingia katika utumishi wa umma kwa masharti ya kudumu,

kwa mujibu wa Sera ya Ajira Menejimenti na Ajira katika 

Utumishi wa Umma toleo la Pili la mwaka 2008iii. Waombaji Wenye Ulemavu

Uchambuzi wa maombi ya watu wenye Ulemavu ulifuata vigezo 

vyote vya mwaka wa kuhitimu na umri wa kuzaliwa,

vilivyooneshwa kwenye kipengele cha (i) na (ii). Hata hivyo, vigezo 

hivi vilitumika kuwashindanisha waombaji wenye ulemavu peke 

yao, kwa kuzingatia takwa la Sheria ya Watu Wenye Ulemavu Na.

9 ya mwaka 2010, kifungu cha 31 (1)-(3). Uchambuzi huu 

ulifanywa kwa ushirikiano na Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana,

Ajira na Watu wenye Ulemavu. 

Ndugu Wanahabari

Mchakato wa uchambuzi wa maombi ya ajira ya Kada za Afya na 
Ualimu ulizingatia utaratibu ufuatao:-

i. Kwanza, ilihusisha uchambuzi wa moja kwa moja kutoka 

kwenye mfumo wa maombi. Mfumo huu umewezesha 

waombaji wote wenye sifa kupata ajira kwa haki na usawa,

kama yalivyo maelekezo ya Rais wa Serikali ya Awamu ya 

Sita, Mhe. Samia Suluhu Hassan, kwamba Watanzania 

wote wenye Sifa wapate ajira bila upendeleo. Hivyo mfumo 

huu uliwachuja waombaji awali kwa kuzingatia mahitaji ya 

kibali cha ajira kilichotolewa, ukamilifu wa viambata 

vilivyohitajika kwa mwombaji, na mwaka wa kuhitimu 

waombaji; na 

ii. Pili, uchambuzi wa kina ulifanyika ukihusisha pia uhakiki 

wa nyaraka za maombi yaliyopata uzito wa juu, kulingana 

na vigezo vilivyowekwa.

2. KUHUSU UZINGATIAJI WA MAHITAJI NA MSAWAZO 
SAWA WA WATUMISHI

Ndugu Wanahabari

Upangaji wa watumishi wa Kada za Afya na Ualimu katika Vituo 

vya kutolea huduma za Afya na shule, umezingatia mahitaji ya 

watumishi katika mikoa husika. Kutokana na juhudi za 

Mheshimiwa Rais wa Awamu ya Sita, Mhe. Samia Suluhu 

Hassan, katika kufanya maboresho makubwa ya Sekta ya Afya, 

upangaji wa watumishi wapya umezingatia mahitaji ya 

watumishi katika Halmashauri zenye Hospitali mpya, Vituo vya 

Afya vipya, na Zahanati mpya zilizokamilika ambazo 

zimeshindwa kutoa huduma za msingi, kutokana na kukosa 

watumishi wenye sifa, pamoja na Halmashauri zenye upungufu 

mkubwa wa watumishi hao. Aidha, kwa upande wa kada za 

Ualimu, utaratibu wa upangaji ulizingatia mgawanyo wa nafasi 

kwa kila somo, na kiwango cha Elimu kulingana na hitaji la 

kibali. 

Mchakato huu wa ajira umetoa fursa kwa waombaji kutoka 

mikoa yote ya Tanzania, hivyo basi upangaji wake umezingatia 

uzalendo na utamaduni wetu, kuwa kila mtanzania anaweza 

kufanya kazi mahali popote nchini.

3. WAOMBAJI WALIOKIDHI VIGEZO NA KUPANGIWA 
VITUO

(a)Waombaji wa Kada za Afya

Ndugu Wanahabari

Kwa upande wa kada za Afya, Waombaji wenye sifa waliokidhi 

vigezo na kupangiwa vituo vya kazi ni 6,876 wanawake ni 3,217

sawa na asilimia 46.8 na wanaume ni 3,659 sawa na asilimia 

53.2 wakiwemo wenye ulemavu 42 sawa na asilimia 0.61 

kutokana na uchache wa waombaji wenye sifa wa kundi hilo.

Aidha, nafasi 736 kada za Afya zilikosa waombaji wenye sifa. 

Kada hizo ni Daktari wa Meno (50), Tabibu Meno (43), Tabibu 

Msaidizi (244), Mteknolojia Mionzi (86) na Muuguzi- ngazi ya 

cheti (313). Kada hizi zitarudiwa kutangazwa ili kupata waombaji 

wenye sifa watakaojaza nafasi hizo.

Ndugu Wanahabari

Mchanganuo wa idadi ya wataalamu wa Kada za Afya waliopata 

nafasi za ajira umeoneshwa kwenye Jedwali la 1.


(b)Waombaji wa Kada za Ualimu

Ndugu Wanahabari
Kwa upande wa kada za Ualimu, Waombaji wenye sifa waliokidhi 
vigezo na kupangiwa vituo vya kazi ni 9,800 ambapo jumla ya 
walimu 5,000 wamepangwa shule za Msingi na walimu 4,800
Shule za sekondari, wakiwemo walimu wenye ulemavu wa shule 
za Msingi na Sekondari 261.
Kati ya Walimu 5,000 wa shule za Msingi wanawake ni 2,353 
sawa na asilimia 47.06 na wanaume ni 2,647 sawa na asilimia 
52.94. Kwa upande wa walimu 4,800 wa Shule za sekondari
wanawake ni 1,289 sawa na asilimia 26.85 na wanaume ni 
3,511 sawa na asilimia 73.15. Aidha, walimu wenye ulemavu 
261 wa shule za Msingi na Sekondari walioajiliwa ni sawa na 
asilimia 2.66 ya walimu wote walioajiliwa wakiwemo wanawake 
84 na wanaume 177. Napenda ieleweke pia kuwa, kwa walimu 
wa sekondari tumetoa ajira za walimu wa sayansi kwa asilimia 
76 ya nafasi 4,800 tulizopewa.
Ndugu Wanahabari
Mchanganuo wa idadi ya walimu waliopata ajira kwenye kada 
mbalimbali za ualimu umeoneshwa kwenye Jedwali la 2.


4. SHUKRANI KWA MHE. RAIS

Ndugu wanahabari

Tunamshukuru sana Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa 

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuendelea kutekeleza 

sera ya elimu bila ada, ambapo pamoja na mambo mengine,

imepelekea watoto ambao walikuwa hawawezi kusoma kutokana 

na kushindwa kulipiwa ada, kwenda mashuleni. Kutokana na 

ongezeko la wanafunzi kupitia sera hii, uhitaji wa walimu na 

miundombinu ya madarasa umeongezeka. Katika kukabiliana 

na changamoto hii, kwa kipindi cha miezi 15 aliyokuwepo 

madarakani, Rais wetu mpendwa ametuwezesha kujenga 

madarasa 15,000 kupitia fedha za mkopo wa IMF, na kutupatia 

kibali cha kuajiri watumishi wa elimu 9,800 na wa afya 7612.

Aidha, katika mwaka 2020/21 Serikali iliajiri watumishi 23,000

kada ya elimu na afya. Hatua hizi zinazochukuliwa na Mhe. 

Rais zinastahili kupongezwa sana.

5. MAELEKEZO YA WAZIRI

Ndugu wanahabari

Napenda kutumia fursa hii kutoa maelekezo ya Msingi 

mbalimbali yanayopaswa kuzingatiwa na Waajiriwa na Waajiri.

a. Waajiriwa wapya wote wahakikishe wanaripoti 

kwa Wakurugenzi wa Halmashauri walizopangiwa 


wakiwa na Kitambulisho cha taifa au namba ya 

utambulisho ya NIDA, Cheti halisi cha kuzaliwa,

Vyeti Halisi vyote vya Taaluma na Utaalamu wa 

Kazi vya mwajiriwa, ili vihakikiwe na Mwajiri kabla 

ya kupewa barua ya ajira;

b. Waajiri wote wahakikishe wanapokea vyeti na 

kuviwasilisha baraza la mitihani kwa ajili ya 

uhakiki. Wizara ipewe taarifa mara moja kwa wale 

watakaokutwa na vyeti ambavyo ni vya kugushi 

ili hatua kali zichukuliwe;

c. Waajiri wote wahakikishe watumishi wapya 

waliopangwa kwenye Halmashauri, wanapewa 

barua za ajira, na kuripoti kwenye vituo 

walivyopangiwa tu, na si vinginevyo;

d. Mwajiriwa

mpya

atakayechukua

posho

ya 

kujikimu, na baadaye asiripoti katika kituo chake

cha kazi alichopangiwa, atachukuliwa hatua

stahiki kwa mujibu wa sheria;

e. Waajiriwa wapya ambao hawataripoti katika vituo

walivyopangiwa ndani ya siku 14, kuanzia tarehe

ya tangazo hili, watakuwa wamepoteza nafasi zao

ambazo zitajazwa na waombaji wengine wenye sifa,

waliopo kwenye Kanzidata (Database) ya Ofisi ya

Rais – TAMISEMI;

f. Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa

ambazo

Waajiriwa

wapya

wamepangwa,

wahakikishe wanawapokea Waajiriwa wapya na 

kuwawezesha kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, 

Taratibu na Miongozo ya Utumishi wa Umma, na

baadaye kutoa taarifa ya kuripoti kwao. Taarifa za

kuripoti waajiriwa hao zijazwe kwenye mfumo wa 

kielektroniki (ajira.tamisemi.go.tz), baada ya kila

mtumishi kupokelewa na kukamilisha taratibu;

g. Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa 

wanaelekezwa kukamilisha taratibu za ajira

haraka, ili waajiriwa wapya waingizwe kwenye 

mfumo wa taarifa za kiutumishi na mishahara 

(HCMIS) mapema iwezekanavyo;

h. Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wote 

wa Halmashauri,

kuhakikisha 

wanatekeleza 

maagizo ya OR-TAMISEMI yaliyotolewa kwenu 

Mwezi Machi, 2022, ya kuhakikisha mnafanya 

msawazo wa IKAMA ya walimu wa Shule za Msingi 

na Sekondari, ndani ya Mkoa na Halmasgauri 

kabla au ifikapo tarehe 30 Juni, 2022. Tekelezeni 

kwa biddi maelekezo hayo ili kuhakikisha shule 

zinakuwa na uwiano mzuri wa walimu, na taarifa 

ya utekelezaji iwasilishwe kabla au ifikapo tarehe 

15 Julai, 2022. OR-TAMISEMI haitasita 

kumchukulia hatua Mwajiri ambaye hatatekeleza 

maelekezo haya ya kufanya msawazo wa walimu katika kuleta uwiano wa mwalimu, na wanafunzi 

wa 1:60 ulioelekezwa; 

i. Tunawaelekeza Wakuu wa Shule na Walimu 

Wakuu kushirikiana na Bodi zao za shule ili 

kufuata miongiozo ambayo Wizara imetoa kwa ajili 

ya michango ya wanafunzi wanaoendelea na 

masomo. Hatua kali zitachukuliwa kwa Mkuu wa 

Shule au Mwalimu Mkuu yeyote ambaye ataenda 

kuinyume na miongozo iliyotolewa na Serikali; 

na

j. Walimu waliopo kazini na Waajiriwa wapya,

kuhakikisha wanafundisha wanafunzi kwa weledi,

na bidii ya hali ya juu kwa kuzingatia kalenda ya 

ufundishaji iliyopo. Wakuu wa Shule, Waratibu 

Elimu Kata, Maafisa Elimu wa Halmashauri na 

Mikoa yote nchini kufuatilia ufundishaji wa kila 

siku darasani, na kujiridhisha kuwa wanafunzi 

wanapata umahiri unaotarajiwa kwenye ngazi 

mbalimbali za elimu ya Msingi na Sekondari.

Aidha, Watumishi wote wa kada za Afya nchini, 

wanaoendelea na utumishi, na walioajiriwa wapya,

kuhakikisha wanawahudumia wananchi kwa weledi na 

upendo wa hali ya juu, kwa kuzingatia Sheria, kanuni 

na miongozo ya utoaji bora wa huduma za afya nchini.


Ndugu Wanahabari

Majina ya waombaji wote waliopangiwa vituo vya kazi

yanapatikana katika Tovuti ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI

www.tamisemi.go.tz.

Asanteni kwa kunisikiliza.

Innocent L. Bashungwa (Mb.)

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI
Where do you want to donate?

Traktir Kopi
Bank BCA - An. Asep Saepul Anwar/ Rek - 648xxxx
Treat the creator to coffee by giving a small donation. click the arrow icon above

Chapisha Maoni

Copyright ©BongoLife - All rights reserved.

Redesign by bloggun.xyz
Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
More Details