SINDIMILA SEHEMU YA 01-04

HADITHI: SINDIMILA
MTUNZI: JAMES JAMES
CONTACT: 0752678890
SEHEMU YA KWANZA

Mila Mila mila. Mila ni kitu kilichotawala sana miaka iliyopita,. Hasa miaka ya 1990,1989,87 kurudi nyuma wazee waliwaonya sana watoto na hata wajukuu wasije kukiuka Mila zao kitu ambacho kingepelekea yeye kuumia ama jamii nzima kudhulika kwa wakati huo ama wakati ujao.
sindimila ni hadithi inayozama zaidi katika kuelezea mila na umiukwaji wake ni hadithi iliyobeba ukweli ndani yake ungana nami katika hadithi hii tuburudike pamoja..

ENDELEA.
"Kaka sam kaka sam, we kaka sam fungua mlango," nilisikia sauti nje ikiniita na kuniomba nifungue mlango. Niliitambua sauti lakini nilikaa kimya kama vile sijaisikia.
"We kaka sam hivi unafanya nini humo ndani hebu fungua mlango" alirudia tena kuita huku wakati huu akiugonga mlango kwa fujo sikutaka kupuuza tena ilinibidi nikafungue mlango ili nisikilize shida yake.
"Naam unasemaje" nilijikuta nikipata mshituko baada ya kuufungua mlango kwani uso kwa uso nilikutana na mdogo wetu wa mwisho merinda akiwa ametapakaa damu mwili mzima.
"Heeeh!! We vip mbona uko hivyo??" Nilimuuliza lakin swali langu halikujibiwa bali alinisukuma na akaingia ndani.
"We Melinda" umezitoa wapi hizo damu nilimfata kumuuliza lakin nilikua nishachelewa kwani aliingia chumbani kwake na akajifungia kwa ndani.
"We Melinda, Melinda" niliishia kuita tuu wala sikupata majibu.
"Mmmh mitoto ya sikuhizi hata adabu imekosa, sasa sijui hizo damu kazitoa wapi daah aya" nilijiongelea huku nikipandisha mabega juu na kuchanua mikono, sikutaka kulifatilia sana jambo hili hivyo niliendelea na mambo yangu.
"Nisijeonekana mbea mie" nilijisemea huku nikitoka nje na kutembea tembea nilienda hadi nyuma ya uzio wa nyumba yetu ooooh masikini wee mama uliniachia haya matoto kwa ninieeeh eeeh leo ndo nimekoma sijui nilifanya nini mimi kwa hawa watoto sasa haya mambo nilijikuta nikikaa chini bila kujua kwani tukio hili lieminyong'onyesha mwili wote kutegemea kuona nilochokiona kwani mbwa wa nyumbani kwetu ambaye ninampenda sana alikua ameuwawa,
Eeeh melinda ndo umefanya nini hiki sasa Nililama huku nikiwa nimekaa pale chini nilijikuta nikkwa mnyonge sana kwan mbwa huyu ameuwawa kikatili sana.
nikiwa bado nimekaa pale chini nilishangaa kutomuona yule mbwa tena alipotea katika mazingira ya kutatanisha nilishituka sana, ikanibidi kuondoka sehemu ile kwani tayari si mahali salama kwangu
Nilienda moja kwa moja ndan kwa lengo lakumwadhibu Melinda lakin haikuwa hivyo nilishindwa kumfiki kutokana na kuwa ameufunga mlango wa kuingilia chumbani kwake
****** ********** *********** **********
Like ukurasa huu wa jumburawahadithi_tz ili uwe wakwanza kusoma hadithi zinazorushwa katika ukurasa huu punde tuu zinapopostiwa.

******* *********** ********** **********
Nilibaki kufokea nje tuu kama mbwa aliyefungiwa ndani ya wavu hata hivyo sikuwa muda ulizidi kwenda na sikuwa na mtu wa kumweleza kwani pale nyumbani tulikua tukiishi watatu pekee ikiwa ni mimi na wadogo zangu wawli Melinda na Sebastian ambaye alikwenda kwa mjomba kumsaidia kulima hivyo nyumbani tulibaki mimi na huyu Melinda, muda ulizidi kwenda hatimaye siku,wiki na hatimaye mwezi huku tukingojea kuona tukio linaloweza kujitokeza lakini hatukuweza kuona tukio lolote la kutisha pale nyumbani

"Seba"
"Naam kaka"
"Njoo hapa mala moja"
"Naam" 
"Nimekuita hapa ili nikwambie kilichotokea hapa wakati haupo, Naimani Ni juma zima Sasa tangu umeludi hapa nyumbani ila hujawahi kumuona mbwa wetu hapa nyumbani" 
"Aaah mie sijui"
"Bwana dada yako alimuua yule mbwa
"Weee kwanini sasa" 
"Ndo hivyo dada ako alimuua na hapa nilipo naishi kwa mashaka masahaka tuu sijui kitakachotokea.
"Kwanini useme hivyo" aliuliza seba
"Yule mbwa alikufa lakini cha ajabu nikuwa mzoga wake haukuonekana tena.
"Kivipi mbona sikuelewi??" 
"Ule mzoga ulipote kwa mazingira ya kutatanisha tena mbele ya macho yangu.
"Aaaah we kaka acha kunidanganya bhana kowahiyo umeona leo unidanganye, yaani kuniita kote huko unaniambi mbwa kauwawa afu kapotea kwa mazingira ya kutatanisha daah we kaka inabidi ukapimwe siyo bure. Alisema seba huku akiondoka
"Seba mi sidanganyi bhana nikweli kabisa nahisi kuna hatari mbele yetu." Nilisema huku nikiwa nimeshika mkono seba lakini aliuchomoa kwa nguvu kisha akaondoka. Alienda huku akilalama kuwa alifikili namwitia jambo la muhimu kumbe Ni upuuzi mtupu..

     ****** ****** ********* ********** ******

Like ukurasa huu wa jumburawahadithi_tz ili uwe wakwanza kusoma hadithi zinazorushwa katika ukurasa huu punde tuu zinapopostiwa

      ******* ********* ********* ***********

"Sam, Sam," ilikua ni sauti ya mama akiniita
"Naam" 
"Mbona umejiinamia chini namna hiyo?"
"Mama wanao wamenichosha"
"Tuachane na hayo amka uwazuie wasiukate ule mti pale njiani hebu angalia wahi uwazuie wanampango wa kuukata ili wapitishe bara bara hapo"
"Mama waache waukate kwani mti wenyewe sio wakwetu acha waukate tuu. Nilisema huku nikiendelea kujiinamia chini.
"Sam nakuambia nenda kawazuie kuukata ule mti" safari hii ilikua ni sauti ya baba. Niliinua kichwa kuwatizama niligundua wamekasilika sana sura zao zilijaa mikunjo inayosababishwa na hasira.
"WE SAM HEBU AMKA UKAWAZUIE KUUKATA ULE MTI WE UNASEMAJE" safari hii waliongea wote huku wakitoa sautj zilizo na ngurumo za ajabu. "Eeeeeeh!!!! Nilishituka kutoka usingizini huku nikitweta kwa kas mithili ya mwanariadha akimbiaye mbio ndefu mapigo ya moyo yalikua kasi sana na jasho lilinitililika kama maji..

 "Daah mindoto mingine bhana inaweza ikasababisha kifo sa ndoto gani za hivi kama si kuuwana huku" nililalama huku nikikunja mkeka wangu na kuviingiza ndani.

Jioni niliingia mtaani kupata kampani japo nibadili mawazo.
Nilipita kando ya mti ambao niliuota mchana huo "sam uwazuie wasije wakaukata huo mti" ilikua ni sauti iliyojiludia kichwani mwangu niliutizama mti huo mkubwa ambao ulionekana kuwa wa kawaida tuh kama miti mingine sikutaka kulifatilia sana swala hili hivyo nikaamua kuendelea na safari zangu.
 Siku hiyo nilirudi nimechelewa Sana giza lilikua limekwisha chukua nafasi yake nilifika hadi maeneo ulipo mti huu mkubwa niliutizama nikaona maajabu yake mti huu ulio yesha sula za watu wengi sana nilstaajabu kwani ni mala yangu ya kwanza kuona kitu kam kile.

"We sam" nilisikia sauti ikiniita kutokea mgongonj kwangu huku mtu huyu aliyeniita akiambaganisha na kunishika begani niligeuka nikakutana na sura iliyofanana na mimi kwa kila kitu japo kuwa yyeye alieonekana kuwa mtumzima kidogo.
"We ninani nambona ufanane na mimi." Niljikakanua nikauliza swali liliilo mfanya mtu huyu atabasamu kidogo kisha akanijibu mimi naitwa sam pia nilikua mlinzi wa mti huu miaja hamsi iliyopita na mimi ni wewe japo kuwa wew ni mtu wa Sasa na mimi mtu wa zamani jukumu lako Ni kulinda huu mti kuna watu watakuja kuu kata huu mti. Kama ilikua hujui mti huu ndiokilakitu hapa kijijini kwenu mti huu ndio mti ulioshikilia mhimili wa Kijiji kizima inakupasa kuulinda kwani mti huu ukipotea na Kijiji chenu kitapata madhala makubwa san.
Mtu huyo alipomaliza kusema vile tuu akatoweka jambo lilo nifanya nikimbie bila kuangalia nyuma.

HADITHI: SINDIMILA
MTUNZI: JAMES JAMES
SIMU: 0752678890
SEHEMU YA PILI

ILIPOISHIA
"We sam" nilisikia sauti ikiniita kutokea mgongoni kwangu huku mtu huyu aliyeniita akiambatanisha na kunishika begani, niligeuka nikakutana na sura iliyofanana na mimi kwa kila kitu japokuwa yeye alionekana kuwa mtu mzima kidogo.
  "Wewe ni nani na mbona ufanane na mimi?"
Niljikakamua kumuuliza swali lilimfanya atabasamu kidogo kisha akanijibu 
" Mimi naitwa sam pia nilikuwa mlinzi wa mti huu miaka hamsini iliyopita na mimi ni wewe japokuwa ni mtu wa zamani" 
 Jukumu lako ni kulinda huu mti kuna watu watakuja kuukata huu mti kama ulikuwa hujui mti huu ndio ulioshikilia mhimili wa kijiji kizima inakupasa kuilinda kwani mto huu ukipotea na kijiji chenu kitapata madhala makubwa.
 Mtu yule alipomaliza kusema vile tuu akatoweka jambo lililonifanya nikimbie bila hata kugeuka nyuma..

ENDELEA....

Nilikimbia hadi nyumbani na ndipo nilipogeuka nyuma kuangalia kama kuna mtu ama kiumbe yoyote anayenifuata nilipojilidhisha kuwa hakuna mtu anayenifuata ndipo nikagonga mlango ambao hata dakika haikupita ukafunguliwa alikuwa ni seba ndiye alinifungulia mlango.
 Kitendo cha kufungua mlango tuu niliingia ndani huku nikihema kwa kasi sana kitu kilichomfanya seba achungulie nje ili kuona nini ninachokikimbia eeeh nahisi ndo yalikua malengo yake hasara kujua nini ninachokikimbia.
 Nilikiendea kiti kinyonge huku nikiendelea kuhema kwa nguvu ili kutafuta pumzi iliyopotea wakati ninakimbia.
 Seba alimuandalia kwa muda kisha akanifuata pale nilopoketi.

      ******** ******* ******** ********* 
Like page ya Jumbura wa hadithi_tz ili uwe wa kwanza kupata hadithi zinazorushwa katika page hii pindi tu zinapo positiwa 

  "Vipi kaka mbona kama unakimbizwa hivi" aliuliza seba swali lililonikera na kuamua kuondoka na kwenda chumbani kwangu 
"Kaka sam, kaka sam nilimuacha akiendelea kuita huku mimi nikizidi kuzipiga hatua kuelekea chumbani kwangu.
 "Nitakueleza baadae nikitulia saivi siko sawa" nilimwambia vile ili kumtoa hofu na asijisikie vibaya huku nilifungua mlango wa chumba changu niliingia na kujibwaga kitandani huku nikivuta kumbukumbu za tukio lile lililonitokea muda si mrefu
 "Aaaah kwani ni kina nani wanaokuja kuukata mti ule, lakini sinimti kama miti mingine mbona niulinde unamaana mimi ndio nimekua mlinzi wa miti wakawatafute mali asili waje kuilinda miti na si mimi.
 Niliwaza huku nikijigeuza huku na huko.
 
"Wasinisumbue mti mti mti ukilala mti ikienda kutembea mti khaaa hadi kelo.." nilitamka kwa sauti ya chini niliyoamini kuwa nasikia mimi peke yangu wakati nikiendelea kuwaza vile macho yangu yalianza kukosa uwezo wakuona kila nilipojitahidi kuyafumbua ndivyo kiza kilizidi kuchukua nafasi kwenye macho yangu nilianza kusinzia taratibu kama teja aliyejifunga madawa ya kulevya
  "Sam huu ni wakati wako sasa kulinda kijiji chako" hakikisha unalitiza hilo na usipofanya hivyo mtaangamia nilisikia sauti ikinisemesha ikitokea nyuma yangu nilipogeuka nilimkuta bwana yule yule tuliyemaliza kuongea naye muda mchache uliopita na akanionya kuhusu mti ule.
  "Kwani ule mti una thamani gani hapa kijijini na mbona wasiukate kama wataukata ili kupitisha barabara mi sioni sababu ya kuwazuia hapa kijijini kwetu hakuna barabara itakua ni bora zaidi ili kuepusha mengi mabaya na kupata mengi mazuri" ni kama maneno yangu yalimtia hasira kwani hata sikuona ni namna gani alivyo nifikia nilijikuta nikiwa chini huku akiwa amenikaba 
 "Mazuri gani unayoyazungumza wewe" alifoka huku akiwa ameendelea kunikaba nilijikuta nikitetemeka kwa woga bwana yule alichomoa upanga uliokuwa uking'aa mithili ya kioo kilichomlikwa na mwanga wa jua. 
 "Unakubali ninachotaka ama nikuue" alisema bwana yule aliekuwa ameunyoosha upanga wake juu tayari kuushusha.

    ********** ************* ***************
Like page ya jumburawahadithi_tz ili wa kwanza kupata hadithi zinazorushwa katika page hii punde tuu zinapo positiwa

"We sam mbona unataka kumuua sasa" nilisikia sauti nyingine ikitokea upande wetu wa kushoto alikua ni mwanamme ambaye pia alifanana sana na mdogo wangu Melinda daah nilichoka mdomo ulibaki wazi na kwa sekunde kadhaa huku nikiendelea kumshangaa mwana mama huyu anayefanana na Melinda 
 Baada ya mama huyu kusema vile nikimuona sam akiniachia.
Mama huyu alinisogelea karibu., Naitwa Melinda alisema mama huyu huku akichuchumaa mahali nilipoanguka kitendo kilichofanya nisogee pembeni kwa woga
 "Usiniogope" alisema mama yule aliyejitambulisha kwa jina la melinda 
 "Mimi ni mtu mwema kwako ila tunachokwambia inapaswa kukifuata vinginevyo utawaumiza wengi. Ngoja nikupe kisa kidogo maana najua unamaswali mengi il naamini kupitia kisa hiki maswali yako yatapata majibu
 "Kwanza kabisa naimani unashangaa nikwanini wewe unafanana na kaka yangu ambaye amejitambulisha kwako mimi sio melinda na wala kaka yangu sio sam kama tulivyo kueleza hapo awali mimi naitwa aheda na huyu ni mume wangu anaitwa kidai sisi tuliwahi kuishi hapa miaka iliyopita huko nyuma,. tulifanya kosa ambalo hadi wakati huu bado halijasamehewa.
 Nakumbuka ilikuwa ni siku moja nilipokuwa nachanja kuni nikiwa na mume wangu pamoja na mtoto wetu niliyekuwa nimembeba mgongoni alijitokeza bwana mmoja mfupi aliyetaka kunidhuru mimi pamoja na mtoto wetu nilipiga kelele za kuomba msaada kwani mume wangu alikua mbali kidogo ndipo alipojitokeza mume wangu na kuanza kupambana na yule mtu asiyejulikana mume wangu alifanikiwa kumdhibiti yule mtu alimtandika jembe la kisogoni na yule alikufa pale pale alikuwa wa maajabu kwani baada ya kupigwa tuu na mume wangu aligeuka nakuwa mti mdogo ulioanza kumea taratibu na ndio ule mti uuonao pale kijijini.
 Tuliendea nyumbani na kuwaeleza kilichotokea leo na hapo ndipo tulipoambiwa kuwa tumetenda kosa ambalo litasababisha maafa katika jamii kwa wakati ule kwani kiumbe yule tulie muua ni kiumbe wa matambiko ya pale kijijini kifupi yeye ni moja kati ya miungu ya kijiji. Mume wangu endelea" alisema aheda akimtaka na mumewe kusimulia
 "Baada ya kuambiwa vile wazee wa kijiji waliamua kutupa adhabu kwani sheria husema kuwa kila mwenye makosa huadhibiwa na ndivyo ilivyokua tulifukuzwa nyumbani na kuamuliwa kuishi karibu na mti ule ili kuulinda usije ukasababisha maafa kwa watu wengine wasio na hatia kwani kiumbe yule akiibuka hatakua kiumbe mwema tena atakua adui.
 Tulipewa miaka mia ya kuulinda mti huu mpaka pale tutakapo mpata watu wengine kwaajili ya kuwakabidhi majukumu haya.
  Hadi leo huu ni mwaka wa hamsini tukiwa tunaulinda mti huu.
 Sasa nyie sio binadamu mnaulindaje mti ikiwa mlishakua wafu?? Nilipata ujasiri wa kuwauliza kwani nilishaanza kuwazomea.
 Ni kweli usemacho ila hata wewe sio binadamu. Alisema aheda na kunifanya nishituke kwa mshangao.
"Mimi sio binadamu!!!" Niliulizwa
Hahahahahaha ninakutania wewe ni binadamu pia ni jini una pande mbili kwani baba yako halisi alikua ni jini.. alisema aheda huku akionekana kumaanisha anachokisema
 Baba yako alikua akiitwa Suleiman alikua ni miongoni mwa majini walioasi ujinini hivyo akakimbia na kuja kuishi na binadamu na hapo ndipo tulipokutana naye na tunamuomba na kumkabidhi mwanetu amuoe ili kupata nguvu ambazo tulizihitaji leo..
 Baba yako na mama yako walipenda na sana lakini upendo wao ulikatiliwa na jini mwingine aliyetaka kuwauwa wewe pamoja na wadogo zako hapo ndipo baba yako alijitoa kuwateteeni nyie na ndicho chanzo cha kuwapoteza wazazi wenu kwani hata mama yenu pia alipoona baba yenu kazidiwa alienda kumsaidia na hapo ndipo walipofaikk na kuwaacha nyingi.
 na ndio maana umepewa majukumu kama haya tunatambua unaweza hivyochuku upanga ukatetee binadamu wenzio.. alisema kudai huku akinirushia upanga
  Kwahiyo nyie ni babu na bibi" .? Niliulizwa swali lililokosa majibu kwani nilijikuta nipo kitandani na upanga nikiwa nimeshikilia.

HADITHI: SINDIMILA
MTUNZI: SALEH MUSSA
NO: 0746492528/0716272123
SEHEMU YA TATU

ILIPOISHIA....
Baba yako na mama yako waliwapenda sana lakini upendo wao ulikatiliwa na jini mwingine aliyetaka kuwaua wewe pamoja na ndugu zake.
Hapo ndipo baba yako alijitoa mhanga kuwateteeni nyinyi na hicho ndicho chanzo cha kuwapoteza wazazi wenu kwani hata mama yenu alipoona baba yenu amezidiwa alienda kumsaidia. Na hapo ndipo walipofariki na kuwaacha nyinyi,.
  "Ndio maana umepewa majukumu kama haya tunatambua unaweza hivyo chukua upanga umawatetee binadamu wenzio.
 Alisema kidai huku akinirushia upanga, 
"Kwahiyo nyie ni babu na bibi" niliuliza swali lililokosa majibu kwani nipo kitandani na upanga nikiilia..
 Like page yangu ya @jumburawahadithi_tz ili uwe wa kwanza kupata hadithi zinazorushwa katika page hii punde tu zinapo positiwa

ENDELEA...
Nikashusha pumzi kwa nguvu huku nikiangalia mahali nilipo. baada ya kujiridhisha na mazingira niliyopo nikajilaza tena kitandani huku nilifikilia kwani nilichokiota kikionyesha dhahli kuwa yote yanayotokea niyakweli.
 Nikatelemka kitandani kisha nikatoka kupelekea sebleni nilikuta hamna mtu. "Inamaana wote wamesha lala" nilisema huku nikiitazama saa iliyopo ukutani ilionyesha kuwa nisaa tano na nusu usiku. Daah kumbe usiku ushakua mkubwa huu nilijisemea huku nikikaa kwenye kiti mawazo hayakuisha kuhusiana na ndoto niliyoipata muda mchache uliopita.
 
"Iwapo mti huo ukikatwa kijiji chenu kitapata madhala makubwa" 
"Ndio maana umepewa majukumu haya chukua upanga ukawatetee binadamu wenzio" yalikuwa ni baadhi ya maneno yaliyojirudia kichwani kwangu kichwa hakikutulia kabisa kwani niliamini sikuwa naota bali nilikuwa nikiongea na watu hao kweli na wamenikabidhi majukumu hayo...
 Hadi inafika saa tisa sikuwa nimepata hata lepe la usingizi nilijivuta vuta nikatoka nje ili nikapate hewa kidogo.
  "Sam" nilisikia nikiitwa na aliyeniita sikumuona iliniwia ngumu kuitika kwani anayeniita simuoni aliendelea kuniita niliangaza ili kuona kama ninaweza kumuona.
 "Sam niko hapa" sauti ilitokea nyuma yangu nilipogeuka kutizama

   ******** *********** ************* ********
Like page yangu ya Jumbura wa hadithi_tz ili uwe wa kwanza kupata hadithi zinazorushwa katika page hii punde tu zinapo positiwa..

Niliiona sura ya malehemu baba nilipatwa na woga kidogo ila nikajitahidi kuuzuia.
 "Sam mwanangu unafanya nini nje usiku huu" aliniuliza
"Nimetoka kupunga hewa kidogo maana sina usingizi kabisa" nilijibu huku nikiwa nimetizama chini kwani kumuangalia ilikuwa inatisha.
 "Ahaaa umetoka nje ili upunge hewa si ndio, lakini mbona kama kuna tatizo linalokusumbua" alisema baba kwa sauti iliyojaa upole ndani yake.
 "Hapana sina tatizo lolote lile linalonisumbua baba niko sawa" nilisema huku bado nikiwa nimeinamisha kichwa changu Chini
 "Mwanagu mimi sio binadamu tangu nikiwa hai hivyo huwezi kunidanganya kitu, nakuona una tatizo linalokusumbua hebu nieleleze nikusaidie angalau kwa mawazo alisema baba huku alinisogelea hadi nilipkua nimesimama kweli baba sina tatizo lolote lile" 
"Aya ila wewe ni mwanaume jitahidi kupambana" 
"Aya hiyo kazi uliyopewa ndiyo inayokufanya uwaze si ndio."
"Ndio baba, jambo hili linakuwa gumu kuifanya" niliongea huku awamu hii nikijikaza kumtizama usoni mwake nikimuona akitabasamu 
 "Sam wewe sio binadamu wa kawaida una mengi unayomzidi binadamu wa kawaida hebu yaruhusu iliyonayo yafanye kazi sawa mwanangu. Hiyo kazi ni ndogo wala isikuumize kichwa ila endapo kama utashindwa piga kifuani kwako mara mbili nitakuja kukusaidia. Alisema baba huku akionyesha tabasamu na ile sura ya kutisha aliyokuwa nayo ilimuondoka 
"Muda umekwenda sasa nenda ukalale" alisema baba kisha akanipigapiga mgongoni kisha akaondoka kama upepo sikuweza kuogopa kwani matukio kama haya nimeyazoea sasa nikaingia ndani nikapitiliza hadi chumbani kwangu nikajitupia kitandani na sekunde chache baadaye tayari nilikuwa naomba melala fofo..

      *********** ************** **************
Like page yangu ya @jumburawahadithi_tz ili uwe wa kwanza kupata hadithi zinazorushwa katika page hii punde zinapo positiwa..

"Kaka sam, kaka sam" nilisikia sauti ikiniita mlangoni kwangu 
"Nini" niliitika kivivu huku nikiichambua vyema sauti ya mdogo wangu Melinda.
"Saa nne saiv bado umelala tu" alisema melinda baada ya kunisikia nimeitika.
 "Saa nne?" Niliuliza huku usingizi wote ukiniisha.
"We ukidhani ni saa ngapi"
"Ayaaaa hii leo ni kali, seba yuko wapi" nilizungumza huyu nilitoka chumbani.
 "Ameenda shamba" 
 "Na baiskeli je ameenda nayo?" 
 "Ndio alienda nayo" alinijibu melinda huku akinitizama kama ananizarau.
 "We melinda unanitazamaje hivyo kama unanidharau hivyo" 
"Aku mimi nkmekutizama kawaida tuu mbona kwani nkmekutizama vibaya? 
"Aaah tuachane na hayo" 
"Kwani uliitaka baiskeli ya nini?" 
"Kwani baisikeli huwa wanaitumia kufanya nini" niliamua kuondoka nikabeba ndoo ya maji na kopo langu nikaenda kuoga nilioga haraka haraka kwani kuna mahali ninataka kwenda nilitoka bafuni nikajiandaa na kupelekea kijiji cha pili kwaajili ya shughuli zangu za hapa na pale redio yangu ndogo nikiwa nimeishikilia nikiendelea kupata habari mbali mbali za nchi yetu..
 
"Halimashauri ya wilaya ya mbeleji imemuomba barabara na iko njiani kuanza kutengenezwa kwani bajeti ya barabara zima na litajengwa kwa kiwango kikubwa 
 wanakijiji wa wilaya ya mbeleji na vijiji vyake adha yenu inakwenda kutatuliwa nilimsikiliza Mkuu wa wilaya yetu akiongea kupitia redio ya taifa ilionyesha kuwa walikuwa na mahojiano.

Niliitizama saa yangu ya mkononi ikanitaalifu kuwa muda huu ni saa tano kasolo dakika 10 
"Ni muda wa kumbimbilika mtoto wa kiume niliongea peke yangu huku nikizipiga hatua kupelekea kwa jirani yetu kuazima baisikeli ili nifike kwa haraka mahali niendako.
 
 "Karibu mwanangu, karibu sana" alisema mama huyu wa jirani aliyekuwa akifua nguo zake
"Asante mama"
"Sam mwanangu karibu, naona leo umekuja kunitembelea" alisema mama huyu huku akinisogezea kiti ili nipate kukaa. 
"Mama mimi sikai"
"Ila utaondoka ama maana mimi huwa sitaki mtu aje kwangu alafu asikae" alisema mama huyu huku akitabasamu 
"Hapana nitakaa kwa siku nyingine mama leo nisamehe tuu. Naomba nilieleza tuu shida iliyonileta hapa kwako" 
"Shida gani?"

       ************* *************** **********
Like page yangu ya @jumburawahadithi_tz ili uwe wa kwanza kupata hadithi zinazorushwa katika page hii punde tu zinapo positiwa

"Nilikuwa nahitaji uniazimishe baiskeli yako niende kijiji cha pili hapo"
"Huko kijiji cha pili unafuata nini? Aliuliza mama huyu huku akiendelea kutabasamu
"Kuna bwana mmoja tuliyekuwa na makubaliano naye kuhusu mifugo sasa inakwenda kumkumbusha maana anaonekana kama amesahau.
"Ahaaa kumbe, me nilifikili labda unanifuatia mkazamwana maana sio kwa kupendeza huko" alisema mama huyu huku awamu hii akiche wa sauti kidogo.
 
"Sasa sam mwanangu baiskeli aliazima mama wa jirani hapo alikuwa anafuatia mihogo shambani hivyo msubili kidogo tuu atakuwa hapa maana amekwenda muda mrefu nahisi atakua njiani anarudi.
"Sawa mama ngoja nisubiri"
"Eeh uchukue kiti hicho sasa ili uwe unamsubili hapo kivulini sawa mwanangu".
"Sawa mama haina shida" 

Zikapita dakika kadhaa huku ukimya ukiwa imetawala kati yetu.
"Hivi sam mwanangu umeshasikia kuhusu barabara itakayojengwa hapa kijijini" mama huyu akaamua kuuvunja ukimya
"Nimelisikia mama tena hata asubuhi hii walikuwa wanalizungumzia"
"Alafu za chini ya kapet sasa na ule mti mkubwa nao utakatwa alafu huo mti inasemekana kuna shetani linaishi kwenye mti huo.
"Kitendo cha mama huyu kusema hivyo kunanifanya nywele zangu kunisimka kichwani kwani ni leo tuu nimeambiwa maneno hayo kwenye ndoto...

HADITHI: SINDIMILA
MTUNZI: SALEH MUSSA
NO: 0746492528
SEHEMU YA TANO

ILIPOISHIA..
"Heeeh baba huyo anakuja nitakutafufa baadae tongee" Alisema saida huku akiinuka na kuondoka
"Poa haina shida"
"Poa"

Mwenyekiti akafika na nikakaribishwa ndani
"Kijana karibu ndani,pita ukae"
Nikaingia ndani na baada ya salamu nikatakiwa kueleza shida iliyonipeleka kwake.
Aaah mwenyekiti kwanza samahani kwa kuja kwako na mukukukatisha shughuli zako ila mimi kuna jambo moja tu lililonileta hapa kwako jambo lenyewe niii..
Nikajikuta nikipata kgugumizi huku ulimi ukiwa mzito nikaanza kushindwa kutamka maneno nikabaki kumtizama tuu mwenyekiti....

ENDELEA......
"Vipi kijana mbona huongei nini kimekusibu" alisema mwenyekiti na kunifanya nishituke kidogo kwani nilishindwa kujieleza kabisa..
"Samahani mzee wangu tunaweza kutoka nje kidogo ya hapa" nilisema huku nikiitazama mwenyekiti kwa jicho la udadisi
"Kwani ni maswala nyeti hadi ushindwe kusema hapa.?" 
"Ndio mzee ni maswala nyeti kidogo" 
"Basi sawa hamna tatizo" alisema mwenyekiti huku akiinuka na kuongoza njia 
Tuka toka nje ya uzio wa nyumba yake 
"Naamini hapa sasa utakuwa huru kusema kile ulicho taka kusema" alisema mzee huyu huku akishika baadhi ya matete yaliyozungushiwa uzio wa nyumba hii
"Ndio mzee, ni kuhusu hili barabara linalotaka kujengwa"
"Ehe vip unataka wakianza ujenzi upate kazi??" 
"Hapana mzee wangu sihitaji kazi wala nini"
"Ila"
"Ila nahitaji nitoe maoni kidogo kuhusu ramani yenu mliyo iandaa kwamba ni sehemu gani barabara barabara itapita ningeomba michole ramani yenu upya ama mbadili mwelekeo wa barabara yaani mpindishe kidogo ili kuukwepa ule mti mkubwa" nikaona uso wa mzee huyu ukianza kukunjamana na tabasamu alilokuwa nalo swali likapotea dalili zote za kukasikika zikaonekana
"Sasa wewe kijana unatoa maoni kuhusu ramani ya barabara ingali wewe sio mhusika wa kamati ya maendeleo ya kijiji ama umeona sisi wote tuliopo kwenye kamati ya maendeleo hatuna akili timamu si ndio, basi ungekuwepo wewe ili utoe mwelekeo wapi barabara itapita mzee huyu aling'aka huku atikisa uzio wa nyumba yake kitendo kilichofanya niogope.
"Lakini mzee haya yote nayasema kwaajili ya kijiji chetu endapo mti huo utakatwa hapatakuwa na mtu yeyote.. kabla sijamaliza sentensi yangu mzee huyu akanikatisha kwa kunyoosha mkono wake juu
"Kijana unajua nilijua wenda una sababu za maana kunitoa mle ndani ili tuzungumze kumbe ni upuuzi mtupu, kwahiyo kumbe wewe unajua nini kijiji kinahitaji kuliko sisi viongozi wake si ndio. Haya ondoka kabla sijakuchafua ondoka.
"Lakini mzee unavyokataa kunisikiliza hivi maneno yangu utayakumbuka tuu. Nilisema huku nikianza kuondoka kwani mzee mwenyewe amekuwa mgumu kunielewa. Nikaondoka huku nikiwa moyo wangu ukiwa umejaa hasira za kukataliwa jambo nililohitaji.

"WE UNAKWENDA WAPI" nilisikia sauti ya mzee huyu akifoka kwa nyuma, alikuwa akimfokea binti yake ambaye wala hakuwa mwingine bali saida.
"Nakwenda sokoni mama kanituma" saida alijibu kwa sauti iliyojaa unyenyekevu na mzee huyu akaingia ndani ya uzio wa nyumba yake kitendo kilichomfanya saida kupata upenyo wa kunikimbilia..

        ********* ************ **************** 
Like page yangu ya Jumbura wa hadithi_tz ili uwe wa kwanza kupata hadithi zinazorushwa katika page hii punde tu zinapo positiwa
    
"We sam inamaana hunioni kama na kukimbilia wewe ukapunguza mwendo" alisema saida huku akiwa amebakiza mita chache kunifikia nikasimama ili kumsubili.
"Pole, nimesikia mazungumzo yenu wewe na baba" alisema saida nikakaa kimya kwa sekunde kadhaa huku tukitembea
"Sam vipi mbona huongei" aliuliza saida nami nikaendelea kukaa kimya 
"Mmmh au kisa alie kukwaza ni baba yangu ndo maana umenikasilikia na mimi.
"Wala hata sijakasioika na sian muda huo wa kumkasilikia mtu eti kisa mtu fulani kanikorofisha.
"Aya naomba unisindikize sokoni basi kama hujakasilika"
"Kukisindikiza sokoni utakuwa mgumu ninakazi nyingi za kufanya" 
"Lakini nimekuomba eti, naomba unisindikize tafadhali" alisema saida kwa sauti Nyololo ambayo haikuwa na mikwaruzo ya aina yoyote ile nikajikuta nikilegea na kukubali kumsindikiza.
"Ila huoni kwamba baba yako anaweza kuniletea shida akisikia nilikuwa na wewe" 
"Wala isikuumize kichwa kwani hata kipindi naondoka ulikuwa umenitangulia hivyo ni lazima ajue tumeongozana, lakini nimesikia mnazungumzia barabara na mti ambao umependekeza usikatwe kwanini na wakati serikali ndiyo imeamua kupitisha barabara hapo?
"Unajua nini saida kuna mambo yamekua yakitokea mara kwa mara na muda mwingine ndoto muda mwingine nakutana nao uso kwa uso na leo nimetoka kuongea nao kabla sijajua kwenu kifupi tuu nahitimisha mwezi tangu nimeanza kuzungumza nao, saida kijiji hiki kipo hatarini kama hakitapata msaada basi kitabaki kuwa jina tuu kwamba kulikuwepo kijiji fulani.."
 "Kwanini unasema hivyo sam mbona kama sikuelewi na kama ni ndoto wenda zikawa ni mauza uza tuu yanayotaka kukkusumbua ila hazina ukweli wowote ndani yake, hebu achana nazo zitakufanya uonekane kama mwendawazimu kwa watu.
"Hapana saida haya mambo niyakweli kabisa maana kuna vitu nimekuwa nikipewa ndotoni na nikiamka nikakuta ninavyo na richa ya hivyo huwa naongea nao na hata leo hii nimekutana nao na nikazungumza nao."
"Kwa hiyo hao wanaokutokea na unazungumza nao ni kina nani??
"Mara nyingi huja babu na bibi na wakati mwingine huja mama na baba pia" 
"Sasa watu waliokwisha kufa watakutokeaaje tena na mkazungumza."
"Hapo ndipo sijui ila kaa utambua kuna maafa yanakuja endapo ule mti utakatwa."
"Kwani mti wenyewe una nini mbona miaka yote upo vile vile kama miti mingine ilivyo ni kwanini mti huo uskatwe"
 "Saida ule mti ni mti wa kawaida tuu kama miti mingine ila mti huo kuna kiumbe ambaye anaishi ndani ya huo mti. Huo mti ndio umefanywa kama gereza lake na endapo mti huo utakatwa basi tambueni huyo kiumbe atatoka na akitoka kijiji hiki hakitakuwa mahali salama tena.
"Mmhh aya baba me sina la kusema juu ya hilo"
"Lazima uwe nalo saida hili ni letu sote hivi unadhani yakitokea maafa hapa kijijini yatahusisha watu baadhi tuu. kumbuka na sisi ni miongoni mwao wana kijiji...

       *********** *********** *************
Like page yangu ya jumbura wa hadithi_tz ili uwe wa kwanza kupata hadithi zinazorushwa katika page hii punde tu zinapo positiwa

Inatubidi kukatisha maongezi haya kwani tayari tumekwisha ingia sokoni saida akanunua vitu alivyotakiwa kununua na tukaanza safari ya kurudi nyumbani
"Ooh mrembo mambo ilikuwa ni sauti ya moja ya wahuni wa hapa kijijini waliotuzingira ghafla kwani tiyari kigiza kishaanza kuchukua nafasi
Wakaanza kumshika shika saida makalio mara nywele kitendo kilichofanya nichukie

"Mniache mimi ni mtoto wa mwenyekiti" saida alilalama huku alijitahidi kujitoa kwenye mikono ya jamaa mmoja aliyemshikilia 
"Hahaha kwahiyo ukiwa mtoto wa mwenyekiti ndio huwezi kuliwa au? Aliuliza moja ya wahuni swali lililowafanya wenzake wacheke
"Oya huyo dem angu msimbuguzi" nilisema huku nikimshika yule bwana aliye mshika saida aliyenisukuma na kusogea mita chache kutoka kwake
"Una demu wewe hahah aliongea huku akizidi kunizonga
"Oya mmemsikia huyu boya anachosema ete tumuachie huyu duu ni demu wake.
"Ahahahahahahahahah wakacheka wote ka pamoja nikaona wakiandaa silaha zao kwaajili ya kunishambulia daah nikajikuta makamu kuongozana na saida kwani muda si mrefu anakwenda kuyagharimu maisha yangu nikaanza kurudi nyuma ili kutafuta upenyo wa kuyasalimisha maisha yangu lakini hatua chache tuu nilijikuta nikipigwa kutokea nyuma na kuanguka chini kama mzigo saida akapiga ukelele mkubwa sana ulionifanya nihamaki nikiwa bado niko pale pale chini..
 
Ulikua ni ukelele wa kuomba msaada kutoka kwangu na nilipogeuka nikamuomba moja ya wahuni alimchukua saida na kuanza kumvutia vichakani huku nikitizama..

ITAENDELEA..
Haya sasa hatimaye sam ameingia mikononi mwa wahuni huku akiwa na saida je watatoka salama kwenye mikono ya hawa jamaa??
Na vipi kuhusu barabara na mti huo je utakatwa ??
Usikose sehemu inayofuata ili kujua ni kipi kitajili katika mkasa huu pia usisahau kulike na kushea kwenye magrupu mbali mbali ili tuendelee kuwa pamoja... Ahsante na siku njema...

Where do you want to donate?

Traktir Kopi
Bank BCA - An. Asep Saepul Anwar/ Rek - 648xxxx
Treat the creator to coffee by giving a small donation. click the arrow icon above

Chapisha Maoni

Copyright ©BongoLife - All rights reserved.

Redesign by bloggun.xyz
Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
More Details