NAJUTA KUUTUNZA USICHANA WANGU SEHEMU YA 37

NAJUTA KUUTUNZA USICHANA WANGU -37

“ Ni..a….ch.e…….” Nilitamka kwa shida.

Katika bingili bingili nilifanikiwa kumuona. Alikuwa ni Hans.

“ ..ha…nsiii……..”

“ Shiiiii………” Alinipa ishara nisipige kelele. Sikukubali, nilimng’ata mkono.

“ Aaaaaaa…….aaahh…” Alipiga kelele na kuniachia. Nilimsukuma na kutoka nje.Nilifunga mlango kwa nje na kupiga kelele.

Baba na Mama walikuja.

“ Kuna nini?” Aliniuliza baba.

“ Haa…nsi…..hans……” Niliwaambia.

“ Yuko wapi!”

Niliwajibu kwa kunyosha mkono. Wote walitazama chumbani kwangu. Kwa pamoja tulipiga hatua kuelekea chumbani kwangu. Baba alitaka kufungua mlango. Mama alimzuia.

“ Hapana, usifungue kwanza. Tunahitaji kuwa na mashahidi.” Aliongea baba. Wazo lake lilikubaliwa na mama. Walitoka na kwenda kuita majirani.

“ Kuna nini?” Majirani waliuliza.

Baba hakuwajibu, aliwasogeza hadi karibu ya mlango wa chumba changu. Alishika kitasa cha mlango na kuufungua mlango. Hans alikurupuka na kutaka kutoka. Baba alimzibiti, baadhi ya majirani kwa woga walirudi nyuma.

Baada ya kuona baba kamthibiti vilivyo, walienda kumpa msaada. Kwa pamoja walimthibiti na kumfunga kamba.

“ Huyu ni nani?” Aliulza mama Husna.

“ Ni hans! Kwani wewe unamuona nani?”

“ Hans si alikufa?”

“ Hapana, hakufa, ni mchezo walifanya ndugu zake. Walikuwa na malengo yao ya kipumbavu. Mungu mkubwa kawaumbua. Walitaka kuharibu maisha ya mwanagu.” Aliongea baba.

Tulipiga simu polisi kuwaataarifu kilichotokea. Usiku ule ule defender ya polisi ilifika.Walituhoji maswali kadhaa kisha wakamchukua na kuondoka naye.

……………………………………………………………

Asubuhi na mapema, niliongozana na baba kwenda kituoni.

Tulifika.

Tulimuulizia Hans. Ajabu, polisi walikataa kuwepo hans pale. Walituambia hakuna mtu anayeitwa hans ambaye alikamatwa usiku.

“Eeeeeeh!” macho yangu yalitanuka kwa mshangao.

“ Naomba mtoke! Mnaongeza uwingi hapa. Hakuna mtu anayeitwa hans hapa.” Alituambia askari aliyekuwa kaunta.

Baba alinishika mkono na kuniongoza kutoka nje. Tukiwa tunakaribia mlangoni, tulikutana na mkuu wa kituo.

“ Emma …” Aliinita.

“ Abeee…” Niliitika na kumsogelea.

“ Unatatizo gani tena?” Aliniuliza.

“ Tumefika kumuangalia hans! Usiku wa kuamkia leo tulimkamata. Tuliwapigia simu polisi wakaja kumchukua. Lakini tumefika hapa tunaambiwa hayupo.” Nilimweleza. Wakati nikiongea na mkuu wakituo, Askari wa kaunta alikuwa ananongonezana na mwenzake. Muonekano wake haukuwa sawa.

“ Mzee anachoeleza binti yako ni kweli?” Alimuuliza Baba.

“ Ndio, kwa mikono yangu nilimshika Hans na kumfunga kamba. Niliwapigia polisi wakaja kumchukua.” Aliongea baba.

Mkuu wa kituo alituambia tumsubiri kwenye benchi, alimwita Askari wa kaunta na kuingia naye ofisini kwake. Masaaa kadhaa mbele, alitoka.

“Kuna michezo inafanyika hapa! Nimetoa maagizo uchunguzi ufanyike haraka. Na wakati uchunguzi unafanyika kuna Askari mmoja anaitwa Musa, nazani anashirikiana na wazazi wa Hans. Yeye nimesema akamatwe na kuwekwa mahabusu.” Aliongea Mkuu wa kituo.

“ mmmh! Afande Mussa si ndio yule aliyekuja kuchukua mwili wa hans alipojinyonga kule hotelini?” Niliuliza.

“ Ndio, ni yeye, inaonekana hata taarifa alizotoa alipokuja kuchukua mwili wa Hans alidanganya. Alitoa taarifa za uwongo.Nazani atakuwa kahongwa na wazazi wa Hans” Aliongea mkuu wa kituo.

Mkuu wa kituo alitutoa wasiwasi, alituambia twende nyumbani. Alituahidi kushughulikia swala letu .

…………………………

Tukiwa tunatoka kituoni, njiani, simu yangu ya mkononi iliita. Alikuwa mama, niliipokea.

“ Hallloooo….”

“ Njooni haraka nyumbani kwa kina Hans..” Aliniambia na kukata simu. Sikumwelewa anamaanisha nini. Sikushangaa, nilimweleza baba na kwa pamoja tulikimbia kuwahi nyumbani kwa kina Hans . Tukiwa tunakaribia, kwa mbali, tulimuona Hans akipigana na baba yake.

“ Nimefanya kila kitu ulichoniambia? Kwanini ulitaka kuniua tena?” Aliuliza Hans. Alimvaa baba yake. Walishikana na kuangushana chini. Baba Hans alipiga kelele na kuomba msaada.

“ Mzimuuuu…mzimuuuu……” Alitamka Baba Hans.

Majirani wengi walifika.

“ Mzimuuuu…mzimuuuuu…unataka kuniua…” Aliongea Baba Hans.

Majirani waliingia kumsaidia, walimvamia hans. Hans alipokonyoka na kukimbilia barabarani.

“ puuuuuuu……” Aligongwa na gari . Alitaka kuvuka barabara bila tahadhari. Tuliwahi kumuangalia. Alikuwa hatamaniki.

“ jinni….jini…………” Wananchi waliongea. Kila mmoja aliongea lake, wapo waliomwita jinni na wapo waliomwita mzimu. Walijaa kushangaa , nilimsogelea pale chini na kutaka kumshika, nilishindwa, halikuwa hatamaniki. Damu zilikuwa zimemtapakaa. Alikuwa katulia tuli.

Kwa mbali, alitokea Mama Hans, alikuwa akikimbia huku akimuita mwanaye.

“ Mwananguuu…mwananguu……” Aliita huku akilia. Alifika. Alimshika Hans na kumtikisa.

“ Amka mwanangu, amka…Hauwezi kufa kirahisi hivi..” Aliongea.

Akiwa analia na kumtikisa mwanaye, alitokea Martini, naye alikuja mkuku na kuanza kulia. Alimshika Hans na kumlilia.

‘ Mwanangu….Hansiii…unakufaje wakati bado hatujafikia mwafaka? Unakufaje ukiwa haumjui baba yako halisi.” Alilalamika Martini. Maneno yake yaliwaacha watu midomo wazi. Walinongona na kumteta, Martini hakujali ,aliendelea kumlilia Hans.

“ Chanzo cha haya yote ni wewe, wewe mwanamke ndio chanzo cha haya yoteeeee…kuwa Mkuu wa wachawi kuna faida gani? Faida yake ni ipi ? cheo kisichokuwa na mshahara kina faida gani? umesababisha nimempotez mwanangu.” Alilalamika Martini.

Maneno yake yalituchanganya.

“ Kuwa Mkuu wa wachawi kuna uhusiano gani na haya yanayaotokea?” Nilijiuliza moyoni.
………………….

Polisi walifika , waliuchukua mwili wa Hans , walimkamata Martini, Baba Hans na Mama Hans wakaondoka nao.
………………….

Tukiwa tunarudi njiani, nilivunja ukimya.

“ Mmeelewa alichokisema Martini?’ Niliwauliza wazazi wangu.

“ Mimi sijaelewa! Kwa utashi wangu ninachojua chanzo cha haya yote ni bikra yako. Walikuwa wakigombea bikra yako kwasababu zao, hizo sababu sijui ni zipi.” Aliongea baba.

“ Yaani mpaka sasa hamjajua tu…” Aliongea mzee saidi akiwa nyuma yetu. Tulisimama kumsubiri.

“ Kama hamjui ngoja niwaambie ukweli. Ipo hivi, chanzo cha haya yote ni madaraka ya kichawi. Martini,Baba Hans, Mama Hans na Onesmo ambaye ni mkuu wa mochwari ,wote wapo chama kimoja cha kichawi, kwenye chama chao ili mtu awe kiongozi mkuu yampasa kutembea na mwanamke bikra ambaye umri wake ni zaidi ya miaka 26, kwa miaka mingi walimtafuta bila mafanikio. Baada ya kukujua wewe ni bikra na una miaka zaidi ya 26, Baba Hans alimtuma mwanae akutongoze.”

“ Baada ya kukutongoza na kukupata, walipanga mbinu baba Hans akutoe usichana wako ili aweze kuwa mkuu wa chama chao cha wachawi, lakini mbinu yao ilifeli kutokana na matendo ya mama Hans. Mama Hans alitaka kile cheo akichukue hawara yake , ambaye ni Martini , na Martini ndie baba wa kweli wa Hans.”

“ Kitendo cha mama Hans kuingilia kilivuruga kila kitu, kilipelekea mpango wa kwanza kufeli.Wakaenda kwenye mpango wa pili ambao ulihusika na maigizo ya Hans kufa, Baba Hans alimuahidi hans fedha nyingi kama zoezi lingefanikiwa, lakini pamoja na Hans kujifanya kufa, Mama Hans alifanya mipango usichana wako utolewe na Martini, na ndio mana siku ile ulituona tukikufanyia dawa ili Martini akutoe usichana wako, lakini Hans alishtukia mchezo, aliwarubuni watu waliomteka baba hans wakaja kukuokoa.” Aliongea Mzee saidi.

“ Lakini mbona Hans alijinyonga kweli?” Aliuliza baba.

“ Hapana, yale yalikuwa maigizo tu, Afande Mussa ambaye alikuja kuthibitisha na kushusha mwili darini , yupo kikundi kimoja cha kichawi na baba hans, hivyo alifanya yale aliyoambiwa na Baba Hans, alidanganya. Afande musa ni kama yule kijana wa mochwari naye yupo kikundi kimoja na Baba Hans, hivyo walifanya yale waliyoambiwa.”

Maneno haya yalinifanya nikumbuke yale yaliyonitokea hospital, nilipoenda kufatilia swala la maiti ya Hans.Kijan wa mochwari alikuwa ni miongoni mwa vijana waliokuja kunishika ili niingiliwe na Martini

“ Lakini kama hans hakufa! Vipi kuhusu ile maiti? Mbona tumefukua kaburi na kuukuta mwili wake?” Nilimuuliza.

“ Yale ni maigizo tu, ndio mana ule mwili mmeukuta kama ulivyo. Haujoza wala haujaharibika. Ule si mwili, ule ni mgomba tu uliogeuzwa kuwa mwili.” Aliongea mzee saidi.

“ Mmmmh! lakini na wewe ni miongoni mwao. Tena wewe wanakuitaga kiongozi wa mila, bila shaka na wewe ni kama wao.”  

‘ Ni kweli, mimi nilikuwa miongoni mwao, lakini sipo tena. Wanangu wamenitoa uchawi wote na kunifanya mtu safi. Hapa nilipo namjua YESU, nimeokoa na namtumikia. Siku nyingi nilipanga nije niwaambie ukweli wa haya mambo. Nashukuru MUNGU leo nimepata nafasi ya kuwaeleza kila kitu.”

“ mmmh! Kwahiyo haya yote kisa ni madaraka ya kichawi! Yaani kuniharibia maisha kisa madaraka ya kichawi?”  

“ Ndio! Mchawi kwa ajili ya madaraka ya kichawi yupo tayari kwa lolote, na ndio mana walikuwa wanamuhonga mama yako hela nyingi ili watimize azma yao. Walikuwa tayari kufanya lolote lile kwa ajili ya bikra yako.” Aliongea Mzee Said.

‘ Najuta kuutunza usichana wangu! Kama nisingeutunza mpaka leo haya yote yasingetokea.” Niliongea.

“ Hapana mwanangu! Ukisema hivyo unakosea, umefanya jambo sahihi sana kujitunza.Kushiriki mapenzi kabla ya ndoa ni kosa kubwa. Hapo ulipo unabaraka nyingi sana za MUNGU. Wachawi na washenzi waliokuwa wanataka kukutumia vibaya MUNGU kawaumbua na bila shaka alikupitisha kwenye hii ili kukufundisha kitu.” Aliongea Baba.

‘ Anachosema baba yako ni kweli, haujafanya kosa lolote lile. Mshukuru MUNGU majaribu yote yameisha bila uhai wako kudhurika. Tulia na umuombe MUNGU. Yeye atakupa bwana bora ambaye anastahili bikra yako.” Aliongea mama.

“ Na unapomuomba MUNGU akupe bwana usiangalie fedha, angalia mapenzi ya kweli. Fedha sio kitu, fedha ni shetani, kwa ajili ya fedha nimeharibu maisha ya baba yako,na bila aibu nilitaka kuharibu na maisha yako.” Aliongea mama.

“ Hii kauli kila siku naisikia, mnamaanisha nini?” Niliuliza.

“ Ni hivi , niliishi na baba yako kwa amani sana, ila baada ya kukuzaaa tama ya maisha mazuri ilinijia, nilianza kutoka nje ya ndoa kwa ajili ya fedha. Huko nje nilipata magonjwa ambayo yalipelekea kiazai change na cha baba yako vikaharibika, na ndio mana baba yako siku ile alikuambia kuhusu mimi kusababisha yeye kukosa watoto, ni kweli umalaya wangu na tama zangu zimeharibu malengo yake mengi.”

“ Pia kama haitoshi, nilishawishika na Martini pamoja na wazazi wa James kwa fedha,kwa tamaaa zangu niliwafanyia mipango ili wakuoe.Na hii yote mwisho wake ni mbaya, mwisho wake ulikuwa unataka kuharibu maisha yako.”

“ Lakini hela hizo ulifanyia nini cha maana?”

“ Hakuna cha maana alichofanya zaidi ya kujaza mabegi ya nguo ndani. Nazani nilikuonyesha siku ile.” Aliniambia baba.

“ mmmh! Halafu nimekumbuka kitu, katika haya yote wazazi wa James walitaka mwanao anioe, lakini hawakuwa na lengo baya wala ushirikina.”

“ Ndio, Baba yake James aliponishawishi aliniambia tu anataka mwanaye aoe bikra, wala wao hawakuwa na mambo mengi kama baba hans na Martini.” Aliongea Mama.

“ Daaaah! Maskini James.”

………………………….

Siku zilikatika, mwili wa Hans ulizikwa, Baba Hans, Martini na mama Hans walishtakiwa kwa matendo yao. Baba Hans alihukumiwa kunyongwa kwa kushirikiana na mwane kumuua James. Mama Hans na Martini nao walifungwa miaka saba Jela kwa matendo yao ya kishirikina.

Afande Mussa alisimamishwa kazi, Onesmo, mkuu wa Mochwari naye alisimamishwa kazi kwa kosa la udanganyifu na kufanya ushirikina eneo lake la kazi.

……………………………….

Siku zilikatika, niliishia kwa amani sana, Miaka mitatu mbele, nilikutana na mwanaume mwingine aitwae Daniel, tulikutana kanisani, tulianzisha urafiki baadae tukawa wapenzi. Tulifata taratibu zote tukaoana. 

Nampenda sana, naye ananipenda pia, tunaishi kwa amani na furaha zote.Upendo wake umenifanya nisahau mambo yote mabaya ya nyuma.

MWISHO.

Where do you want to donate?

Traktir Kopi
Bank BCA - An. Asep Saepul Anwar/ Rek - 648xxxx
Treat the creator to coffee by giving a small donation. click the arrow icon above

Chapisha Maoni

Copyright ©BongoLife - All rights reserved.

Redesign by bloggun.xyz
Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
More Details