SHEIKH ALIYEOA MWANAUME AKIDHANI NI MWANAMKE AFUTWA KAZI UGANDA

SHEIKH ajikuta ameowa mwanaume Bila kujua na kupelekea kufukuzwa

#HABARI YA KUSIKITISHA.
SHEIKH ALIYEOA MWANAUME AKIDHANI NI MWANAMKE AFUTWA KAZI UGANDA


BONGOLIVES - SHEIKH ALIYEOA MWANAUME AKIDHANI NI MWANAMKE AFUTWA KAZI UGANDA

Huku mjadala kuhusu kama kweli alifahamu jinsia ya bi harusi wake wiki mbili zilizopita alipofanya nikka naye, baraza hilo linasisitiza kuwa kuna dosari kubwa kwa upande wa imam huyo na hastahili kuendelea na kazi yake

Sheikh Mohammed Mutumba anadai kuwa alipata mshtuko wiki mbili baada ya kugundua kuwa mke aliyemuoa aliyekuwa akivalia vazi la hijab kila wakati na anafahamika kama Swabullah Nabukeera alikuwa ni mwanaume anayeitwa Richard Tumushabe.

Ukweli kuhusu jinsia yake ulibainika baada ya polisi kumkamata Tumushabe kwa madai ya wizi wa televisheni na nguo za jirani yake..

"Wakati polisi wakifanya shughuli zao za kila siku, askari wa kike alimkagua sehemu zake za mwili kabla hajampeleka jela. Na kuwashangaza maafisa wa polisi kuwa mtuhumiwa huyo kuwa aliweka nguo katika sidiria ili aonekane ana matiti,"bwana Mugera alinukuliwa.

Sheikh Mutumba - ambaye ni imam wa msikiti uliopo kijiji cha Kyampisi , kilomita takribani 100 (62 miles) kaskazini magharibi mwa mji mkuu wa Uganda, Kampala - alidai kuwa hajafanya naye tendo la ndoa mke wake huyo tangu amuoe kwa sababu alisema kuwa alikuwa ana matatizo ya kiafya yaliyomfanya kuendelea kupata hedhi na ilimbidi amvumilie mpenzi wake.

"Tayari tumemshtaki kwa kosa la kujiigiza kuwa mtu mwingine, vilevile kwa kosa la wizi na kujipatia vitu kwa ulaghai ," bwana Mugera alisema.

Gazeti la Daily Monitor limeripoti kuwa Sheikh Abdul Noor Kakande, ambaye ni kadhi wa ukanda huo (jaji wa kiislamu), amesema kuwa tukio hilo ni la kushangaza sana na halikubaliki, hivyo imam anafanyiwa uchunguzi.

Vilevile Baraza kuu la Sheikh mkuu wa msikiti ambao sheikh Mutumba anaswalia, Isa Busuulwa, amesema kuwa amemsimamisha kazi sheikh huyo kwa heshima ya imani ya kiislamu hivyo hatoruhusiwa kuswalisha katika msikiti wowote ule.

Baadhi ya wanawake nchini Uganda na wao wametowa hisia zao wakisema Imamu huyo kuna kitu anaficha:

"Haiingii akilini kwa namna moja au nyingine, hata kama ni mtu wa kujifunika na tunaelewa waislamu wanajifunika sana.Lakini hawa watu walifahamiana na kupelekana nyumbani ,na kwa muda wa wiki mbili kuna mambo mengi kati ya mume na mke, kuna kuoga,kubadilisha nguo, kuangaliana na mambo mengine mengi"

"Nataka kuuliza huyu imamu hajui utofauti wa mwanaume na mwanamke kwa muda wote wa wiki mbili, ina maana hajawahi hata kumkumbatia?"

Msemaji wa polisi mkoa maalum wa polisi wa Ssezibwa Hellen Butoto amefahamisha BBC kwa njia ya simu kuwa mtuhumiwa bado amehifadhiwa kituo cha polisi Kayunga na amefunguliwa mashitaka

"Sasa mutuhumiwa anasubiri kufikishwa mahakamani kusomewa mashitaka ya kudaganya maumbile yake".

Where do you want to donate?

Traktir Kopi
Bank BCA - An. Asep Saepul Anwar/ Rek - 648xxxx
Treat the creator to coffee by giving a small donation. click the arrow icon above

Chapisha Maoni

Copyright ©BongoLife - All rights reserved.

Redesign by bloggun.xyz
Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
More Details