Mwanafunzi aliyefichwa taarifa za kifo cha wazazi wake na wadogo zake watatu ameambiwa rasmi jambo hilo.

Dar es Salaam. Hatimaye Anna Zambi, Mwanafunzi aliyefichwa taarifa za kifo cha wazazi wake na wadogo zake watatu ameambiwa rasmi jambo hilo.

Mwanafunzi aliyefichwa taarifa za kifo cha wazazi wake na wadogo zake watatu ameambiwa rasmi jambo hilo.

Anna amewasili nyumbani kwao Goba, jijini Dar es Salaam saa 10.30 alfajiri akitokea katika Shule ya Sekondari ya Mather Theresia of Calcuta inayomilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo la Same.
Anna mwenye umri wa miaka 16, alimaliza mtihani wa kidato cha nne na mpaka anawasili nyumbani kwao hakuwa na taarifa kama wazazi na wadogo zake wote watatu walifariki ajalini.

Wazazi wa Anna, Lington Zambi(Baba), Wilfrida Lyimo (mama) pamoja na wadogo zake Lulu, Grace na Andrew walifariki baada ya gari aina ya Noah waliyokuwa wakisafiria kusombwa na mafuriko Handeni mkoani Tanga.

Familia hiyo ilikuwa ikielekea shuleni kwa mtoto wao kuhudhuria mahafali ya kidato cha nne iliyofanyika kabla ya kuanza mitihani ya mwisho.

Mtihani mkubwa uliokuwepo ilikuwa ni namna ya kumpatia taarifa za kuondokewa na ndugu pamoja na wazazi wake. "Alipofika watu wanne wanaume wawili na wanawake na wanaume wawili walienda kumweleza mtoto juu ya kilichotokea, alilia tukaja nae mpaka ndani alipoingia akajilaza miguuni kwa bibi yake akiendelea kulia," amesema baba yake mdogo, Ibrahim Zambi. "Aliongea mengi akilia akasema alihisi jambo hilo na kuna wakati aliamka usiku na alisema mitihani yake amefanya kwa tabu sana." Ibrahim alisema kati ya maneno magumu aliyozungumza wakati akilia ni "Kwanini mliniacha mkuja mnichukue tuondoke wote," "Tunashukuru Mungu tulihofua sana angepata shida kubwa ila amepokea vizuri anaomboleza tu," amesema.

Daktari Doya Frederick aliyepo msibani hapo ameshauri mtoto apumzike na kupitia hatua zote za huzuni ndipo asaidiwe kiimani na kisaikolojia. "Mtu anapopata taarifa za jambo gumu anapitia hatua kadhaa ili akae sawa ndipo asaidiwe kisaikolojia lakini pia ajengwe kiimani. Hatua hizo ni kukataa, hasira, kubishia kwamba haiwezekani lakini baadae kukubali uhalisia," amesema Dk Doya.

Where do you want to donate?

Traktir Kopi
Bank BCA - An. Asep Saepul Anwar/ Rek - 648xxxx
Treat the creator to coffee by giving a small donation. click the arrow icon above

Chapisha Maoni

Copyright ©BongoLife - All rights reserved.

Redesign by bloggun.xyz
Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
More Details