CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu) SEHEMU YA 15

CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu)

MTUNZI: @minnah de Embaccas

SEHEMU YA KUMI NA TANO (15)

Whatsapp :0656282898

ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA NNE: "dokta nini mbona uongei?".aliuza mzee Popati huku mkewe akiwa ametolewa nje apate hewa. "tuambie basi niramu kimempata nini? ".aliuliza vicent huku anamtazama daktari. "nananana.. nasikitika kusema kuwa mgonjwa ametutoka".aliongea daktari kwa kigugumizi lakini aliongea kwakutimiza wajibu wake. "whaaaaaaaaaaaaat".vicent aliongea uku akijibwaga chini kama gunia puuuuuuuuuuuuh!! ENENDELEA.....
Alijibwaga chini puuuuuuuh!!. Huku akilia kwa uchungu, baba na mama yake wakaenda kumbembeleza huku na wao wakilia, baba niram alikuwa kama mtu aliechanganyikiwa alikuwa aelewi afanye nini maana alibaki ameshika kichwa mikono kichwani mdomo kauacha wazi, chozi likimdondoka maskini alitia huruma sana mzee popati, ni binti yake wa pekee kati ya watoto wake wawili aliobahatika kuwa nao. Razaki mpaka muda huo awakumjulisha chochote kwakuhofia kuweza kumchanganya zaidi maana alimpenda dada yake kupita maelezo. Wakati wote huo huko nje mama niram alikuwa asharudiwa na fahamu, ila alikuwa bado ajakaa sawa presha ilikuwa juu hivyo walikuwa wanamfanyia huduma ya kumshusha presha yake, iliyokuwa juu kupita kiasi. Dokta alikuwa ndo anamalizia kuufunika mwili wa niram na shuka la kijani ili amtoe nje kumpeleka monchwari. Ila vicent akaipachua mikono ya wazazi wake waliokuwa wamemkumbatia wakimfariji, akanyanyuka fasta na kuenda kulifunua shuka huku akimtingisha niram. "niram uwezi kuwa na ubinafsi kiasi hicho niram kwanini umeamua kukatisha ndoto zetu?, mbona mimi nimepambana kuupigania uhai wangu ili nisikuache mwenyewe, lakini kwanini wewe umeamua kuniacha mwenyewe whyyyyyyyyyyyyyyyyyyyyy? ".aliongea vicent huku akipiga kelele za maumivu akiendelea kumtikisa. Dokta akamfuata vicent ili amtoe ila mzee popat akamzuia daktari. Akiwa anajuafika kuwa vicent alikuwa ana mapenzi na mwanae kiasi gani.basi daktari alikaa pembeni wazazi wa vicent wakiwa pembeni, kikweli walikuwa wanamuonea sana huruma mtoto wao, awakujua itakuwaje baada ya pale. "niram amka mama, nikuambie kuwa nakupenda sana na sitamani kuwa na mwengine zaidi yako".aliongea vicent huku amemuinua niram akamvuta kwake na kumkumbatia. "vicent mwanangu mwachie mwenzio apumzike kwa amani ameshatutoka aina jinsi".alikuwa ni baba yake niram aliongea akiwa nyuma ya vicent huku akimshika mabegani. Vicent alimtazama kisha akageukia tena niram wakati huo alikuwa ameshamlaza ila amemshika, Mikono yake ,vicent aliendelea kumtazama kwa hasira na kukata tamaa huku macho yakiwa mekundu, mishipa ya kichwa ikiwa imechachamaa. "sawa nakuacha uende kwakuwa wewe ndo umechagua hivyo, ila tambua kuwa sitakusamehe kwa kuniacha mwenyewe wakati unajua ntaishi kwa mateso niram sitakusameheeeeeeee".aliongea vicent kwa uchungu huku analia, akanyanyuka huku akijipachua mikono yake kwa niram ili aondoke lakini ikawa migumu kutoka, akajaribu tena ikawa hivyo hivyo akainua uso kumtazama mara akamuona niram anapiga chafyaaaa. Vicent akapiga kelele kwa furaha maana kile kitendo alikisikia na kukiona mwenyewe kwasababu dokta alitoka kwenda kumuhudumia mama niram, baba niram baada ya kumwambia vicent kuwa amuache mwenzie apumnzike akatoka huku analia akienda nje kuangalia hali ya mkewe maana alijua anaweza kupoteza watu wawili kwa mpigo. Mule alibaki vicent na wazazi wake waliokaa kitanda cha pili wakiwa wamejiinamia huku wanalia. Kwahiyo vicent ndo alieshuhudia tukio lile peke yake. "doktaaaaaaaaa ameamka huku"ilikuwa ni sauti ya furaha kutoka kwa vicent. Wazazi wake vicent wakagutuka kutoka kwenye lindi la mawazo wakakimbilia Kwenye kitanda cha niram, huku mzee popat akija mbio nusu ya kuvunja mguuu akija kwa kasi nyuma akifuatiwa na daktari. Walipofika hawakuamini walichokiona wote walijawa na tabasamu, baba yake alishindwa kujizuia alinyanyua mikono juu huku machozi yakimtoka akamfuata mwanae na kumkumbatia kwa furaha. "imekuwaje hivi hakika Mungu wewe ni wa kutukuzwa siku zote asante kwa muujiza wako nimekuwa daktari kwa muda wa miaka 18 lakini sikuwahi kuona tukio kama hili".aliongea daktari huku chozi la furaha likomdondoka. " vicent mpenzi nashukuru kukuona ukiwa hai siamini".aliongea niram vicent akatabasamu kisha akamfuata na kumbusu. "hii yote sababu yako ningekuwacha na nani sasa".aliongea vicent wote mule ndani wakatabasamu. Mara wakamwona mama niram analetwa na nesi huku ameshikwa mkono akija huku analia alipofika alishindwa kujizuia alipomwona mwanae akatabamu, "mama ".aliita niram, mama yake alishindwa kujizuia akamkumbatia huku akiwa na analia kwa furaha. Basi mule ndani kukawa na furaha isiyo kifani kila mtu akiwa aamini muujiza Mungu aliowatendea.
******
Vanessa alikuwa yupo selo akilia akijutia kwa alichokifanya, kwani alijuta sana na alikuwa ajategemea kufanya vile. "mapenzi hayalazimishwi naimani kila mtu kaumbiwa na mwenza wa maisha yake sasa mimi nilitakiwa nikubali matokeo kuwa vicent hakuwa wangu oooh Mungu nisamehe mimi".alijisemea Vanessa huku analia. Maana Vanessa alivyotoka pale ukumbini akuelewa afanye nini maana alikuwa kama amechanganyikiwa, akafikiria kwa muda akaamua aende kwao. Huko alipofika aliwasimulia wazazi wake kilichotokea wote walikuwa wanalia maana walijua kwa kesi ya mauaji mtoto wao asingepona. Baada ya kuwaadithia akiwaacha ndugu na wazazi wake wakilia, mara wakaingia askari na kumchukua akiwaacha wakina juliana wakiwa wanalia sana. 
Kwahiyo kwa upande wa Vanessa ilikuwa hivyo mpaka kufikia leo kukutwa yupo selo. "najutia sana roby ni mwanaume mzuri na alikuwa akinieleza kuwa ananipenda kwanini nisingemsikiliza, yasingenikuta haya".alijutia sana Vanessa. 
*******
Ilikuwa mida ya jioni. Kuna gari lilifika kituo cha polisi, mara akashuka vicent na niram wakiwa na wazazi wao inaelekea walikuwa hawajafika hata makwao ndo kwanza walikuwa wanatokea hospitalini. Mara baada ya kushuka huku vicent akiwa anachechemea alishikiliwa na niram walifika pale na kutoa maelezo. "Vanessa Msangi ".ilikuwa ni sauti ya askari alikuwa anamuita. "abeee".aliitikia "toka nje".alisema yule Askari huku anafungua mlango. Vanesa alikuwa anashangaa imekuwaje. Na wakati huohuo wazazi wake Vanessa walikuwa wanamletea mtoto wao chakula, wakashangaa mtoto wao ametolewa nje. "upo free wamekuja kukutoa kwahiyo siyo mtuhumiwa tena upo huru".aliongea askari ,wazazi wa Vanessa walishindwa kujizuia waliona kama ndoto walifurahi sana huku mama yake akipiga magoti na kumshukuru Mungu huku wakiwashukuru pia wakina vicent maana hawakutegemea. "vicent na niram nisameheni sana, halikuwa dhumuni langu ila sikuelewa sababu ya kufanya vile naomba muelewe najutia sana". Aliongea vanessa huku analia. Vicent alimfuata na kumfuta machozi. "usilie mimi ndo mwenye makosa sikukuambia ukweli kuwa Sikuwa na mapenzi na wewe nimekufanya kuamini kuwa nakupenda kumbe sivyo, nimekukosea sana vanessa tafadhali nisamehe".vanessa alimtazama kisha akamkumbatia na kutamka. "nimekusamehe kutoka ndani ya moyo wangu". Wote wakafurahi kila mmoja akawa na amani. Baada ya hapo wakatawanyika kwenda makwao wakiwa hawana vinyongo mioyoni mwao. Uhusiano wa niram ukakubaliwa pande zote mbili na wakakubaliana baada ya kumaliza masomo watafunga ndoa bomani, kila mtu na dini yake. "vicent hivi mtoto wetu wa kwanza tutamuita nani?".aliuliza niram wakiwa wamekaa kwenye bustani nzuri kwenye nyumba yakina vicent, huku vicent akiwa amelala mapajani mwa niram. "lazima aitwe jina la kikristo mtoto wa kwanza wa baba".aliongea vicent huku anatabasamu. "sawa baba".aliongea niram huku anacheka, vicent akamtazama kwa muda kisha akamvutia kwake, mara ndimi zinakutana wakapeana juisi nzuri ya denda. Baada ya sekunde kadhaa wakaachiana. Huku wote wakitabasamu. "nakupenda sana malkia wangu, wewe ndo furaha yangu ".aliongea vicent kwa sauti nzito na yenye hisia. "nakupenda pia mfalme wangu wewe ndo kila kitu kwangu ".alijibu niram wote wakatabasamu huku wakikumbatiana, walionekana ni watu wenye furaha sana, walisahau kila kilichotokea na maisha ya amani na upendo yakitawala baina yao,kila siku penzi lilizidi kukua na mapenzi Kati yao yaliongezeka. Mwishoooooo ...

Where do you want to donate?

Traktir Kopi
Bank BCA - An. Asep Saepul Anwar/ Rek - 648xxxx
Treat the creator to coffee by giving a small donation. click the arrow icon above

Chapisha Maoni

Copyright ©BongoLife - All rights reserved.

Redesign by bloggun.xyz
Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
More Details