CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu) SEHEMU YA 12

CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu)

MTUNZI: Minnah De Embaccas

SEHEMU YA KUMI NA MBILI (12)

Whatsapp :0656282898

ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA MOJA: Akamtext whatsapp akaona kimya alivyo angalia vizuri akakuta vicent amemblock "Oooh!! Mungu wangu vicent usinifanyie hivyo".alijikuta anaropoka niram huku mikono kaweka kichwani simu imemdondoka hata kuijali akuijali alivyoangalia pembeni akaona. ENDELEA.....
Alivyoangalia pembeni akaona kile chakula chake alichowekewa na mama yake, alikitazama kwa macho ya chuki kama vile ana ugomvi nacho, akanyanyuka na kukisogelea akakiputaaa chote kikamwagika chini wali pamoja na kipaja cha kuku vyote vilikuwa chini vikivunjikiwa na vipande vidogo vidogo vya sahani ya udongo. Kwakweli alikuwa kama mtu alie changanyikiwa, na kwa bahati nzuri zile kelele za sahani hazikusikika kwa mtu yeyote kwa maana muda ulikuwa umeenda sana watu walikuwa wamelala. Alifikiria sana mwishowe akaamua apande kitandani ajaribu kuulazimisha usingizi kwa maana ulikuwa mgumu kupatikana. 
******
Ulikatika mwezi hatimaye wakina vicent, walikuwa wameshamaliza mitihani kwahiyo walikuwa nyumbani wakisubiria majibu ya kuenda chuo. Wakati wote huo mapenzi ya Vanessa na vicent yalikuwa motomoto, japo hawakuwahi kukutana kimwili,kilikuwa na kipindi cha furaha kwa vanessa, alijiona ni mtu mwenye bahati sana kuwa na mwanaume aliyempenda kwa siku zote. Japo ilikuwa tofauti kwa vicent japo alishaamua kuwa na vanessa lakini niram akumtoka kwenye akili yake. Kuna muda alitamani amtafute kwa njia yoyote hile ila akaona atajipotezea muda wake bure, kwani niram hatoweza kuwa na yeye.basi akaamua bora ajilazimishe kuwa na mwanamke aliyejitolea kumpenda huenda siku moja nayeye atakuja kumpenda na wakaishi kwa furaha, hiyo ndiyo ilikuwa ndoto na vicent kwamba siku moja atakuja kumpenda Vanessa na maisha yataendelea. Nakumbuka ilikuwa siku ya Jumamosi kulikuwa na shamrashamra kwa wingi kwenye nyumba ya kina vicent. Kulikuwa na maandalizi ya birthday ya vicent inayofanyika siku hiyohiyo usiku kwenye ukumbi wa nyumbani kwao humohumo maana kulikuwa na hali kubwa lililojengwa kwaajili ya sherehe mbalimbali. 
Walialikwa watu mbalimbali japo muda ulikuwa bado,ila ndugu wa karibu walifika mapema kuandaa mazingira vizuri japo wapishi walishakodiwa na kuandaa bufee, wapambaji ukumbi pia nao walikuwemo wakifanya kazi yao bila Kusahau kamati ya vinywaji nayo haikuwa mbali,kiukweli wazazi wa vicent walijipanga vilivyo kuhakikisha mambo yanaenda sawa. 
Vanessa na vicent mapenzi yalikuwa motomoto, kiasi kwamba ukiwaona unaweza sema hawa watu hawatokuja kuachana kamwe. Haswa kwa vanessa alikuwa aambiwi asikii yani kifupi alikuwa mtu mwenye kutabasamu wakati wote, kwake kuwa na vicent alijiona ni mtu mmoja mwenye bahati sana.japo kuna wanaume wengi waliokuwa wanamsumbua kwa uzuri na umbo lake matata lakini hakuwajali yeye alikuwa anampenda mmoja tu vicent. Kwa upande wa vicent alikuwa yuko happy, japo muda mwingi alikuwa anamfikiria niram, hakumtoka kwenye akili yake ila aliamua kupiga moyo konde na kuwa na Vanessa kwakuwa alionyesha kumjali na kumpenda kwa dhati. Japo alijua fika kuwa yeye hakumpenda Vanessa kihivyo lakini alijipa moyo atakuja kumpenda na kila kitu kitakuwa sawa. Vicent alikuwa ameshawaalika watu mbalimbali bila kuwasahau mabest zake Richard pamoja na suma. Muda huo alikuwa ndani ya gari akiwemo pamoja na mpenzi wake Vanessa wakielekea mjini kufata keki. "baby inabidi tuende na muda, masaa yenyewe yanakimbia".ilikuwa sauti ya vanessa aliekuwa amekaa pembeni yake akimsihi ."usijali wangu nipo makini sana hii ni saa tisa bado sana". Akijibu vicent huku macho yakiwa mbele akiwa makini na uendeshaji wa gari. "eeeh!! Usijisahau sana utashangaa muda umefika keki bado atujaipata". Alisisitiza vanessa. "usijali my love".aliongea vicent huku akimpachika na kibusu cha shavu, Vanessa akatabasamu kiuvivu huku wakizidi kukata mitaa kuelekea mjini
*******
Niram alikuwa chumbani kwake akijiandaa kutoka kuelekea supermarket kuenda kununua bidhaa za nyumbani kwao. Alivalia baibui lake la kisasa akajipachika na kimtandio chepesi kilicho nakshiwa na maua maua. Akajipulizia kipafyum chake kisichokera akijitazama jinsi alivyopendeza. Alivyoona kuwa yupo sawa alichukua kibegi chake na kutoka kuelekea chumba cha mama yake kilichokuwa jirani na chumba chake. "mama mi nipo tayari nakusubiria wewe tu".aliongea niram akiwa amesimama jirani na chumba cha mama yake. "sawa nakuja sasahivi".ilisikika sauti ya mama niram ikijibu kutokea chumbani, ila ghafla mlango ukafunguliwa akatoka na kumkabidhi pesa. "ila naomba usisahau kubeba maziwa maana yameisha".alisisitiza mama yake. "sawa mama sitasahau, byeee".aliongeza niram huku anatoka kuelekea nje. "byeee ufike salama".alijibu mama niram. "sawa mama".alijibu niram huku anamalizikia kutoka mlangoni na kufunga mlango, akaenda sehemu ya kuegesha magari akachukua gari aitakayo, akamwambia mlinzi amfungulie geti,akaingia ndani ya gari na safari ikaanza. Akaicha barabara ya kwao na kutokomea kwenye barabara nyengine itakayomtoa mpaka barabara kuu. Njiani alikuwa ni mtu mwenye mawazo sana japo kwasasa alishaanza kusahau, ila vicent hakutoka kwenye akili yake alimuwaza kila dakika na Akujua atafanyaje ili kumfikishia ujumbe kuwa anampenda. Aliendelea kukata mitaa na siku ya Jumamosi inakuwa haina foleni basi alifika mapema supermarket. Alipaki gari lake kwenye sehemu ya kuegesha magari taratibu akawa anaingia ndani ya jengo la supermarket, wanaume shingo zilikuwa zinataka kuvunjika kwaajili ya kugeuka kumtazama, aliwaona ila awakapotezea huku tabasamu likichanua usoni mwake bila kuonyesha kuchukia. Alifika ndani akachukua kibaskeli cha kubebea bidhaa, akaanza kuchukua mahitaji yake, alizunguka mpka alipoona Kamaliza ndo akajiandaa ili aondoke, mara akakumbuka kasahau maziwa. Arirudi mpaka sehemu yanapokaa akawa anayechukua, gafla kutupa macho mbele hakuamini alichokiona moyo ulipigaa paaah!! Alimuona vicent akiwa amesimama na mwanamke wakiwa wamekumbatiana wanasubiri keki yao iliyokuwa inawekwa kwenye box, ilikuwa bonge la keki. Lakini vicent hakumwona. Niram alisogea mpaka karibu yao huku sura ameiziba na Mtandio akijifanya anaendelea kuchagua mahitaji. Alisimama hatua chache na walipo wao huku akiwaangalia kwa jicho pembe. Akawasikia wakiongea. "yani baby nyumbani kwenu leo kutakuwa na Shangwe siyo za za nchi hii,mtoto tena kazaliwa".aliongea vanessa huku akimugemea vicent kwenye bega lake la kushoto. "sana mkewangu mtoto wapekee tena nnazaliwa".alijibu vicent kwa mbembe. Kiukweli niram hakuweza kuendelea kubaki pale kwani alijisikia wivu na maumivu mno. Alienda mapokezi akalipa akachukua mizigo yake akaiweka ndani ya gari akaingia akawasha gari huyo akaondoka zake kwa spidi kali. 
******
Ilikuwa ni mida ya saa kumi na mbili jioni. Niram alikuwa ameshafikia nyumbani kwao. muda wote alikuwa anawaza tukio lililotokea kule supermarket kiukweli alizidi kuchanganyikiwa, baada ya kufikiria sana akanyanyuka kitandani na kutoka mpaka sebuleni alimkuta mama yake amekaa na msichana wake wa kazi wanaangalia tv. Niram alifika akakaa.lakini kichwani kwake alikuwa ameshafikiria jambo, "wewe mbona upoupo tu kama vile hauko sawa".ilikuwa sauti ya mama yake, ambaye alipomuangalia akaona kuwa kuna kitu kinamsumbua mwanae. "we acha tu mama yani nina tatizo kweli,lakini sijui kama utaweza kunisaidia".aliongea niram huku akimuangalia mama yake kwa macho yenye uitaji wa kitu fulani. "mmh! Kitu gani hicho mpaka uwe na wasiwasi kuwa sitakusaidia?".aliuliza mama yake kwa umakini. Wakati wote huo msichana wao alikuwa bize kuangalia runinga. "mama rafiki yangu ana birhday yake leo, sasa aliniambia niende nikamkubalia ila nilijua sitaenda, lakini leo meseji zake nyingi zinanisisitiza niende nisikose na nikiangalia alishawahi kunisaidia nilipobanwa na pumu shuleni".aliongea niram kwa huruma kupita kiasi. Mama yake alimtazama kisha akaongea. "hivi unajua kuwa unataka kunitafutia matatizo kwa baba yako? Akijua kuwa nimekuuruhu kutoka usiku nyumbani unataka aniue sijui". Aliongea mama yake niram huku akimtazama mwanae. Niram hakuwa na cha kujibu mpaka hapo alikuwa ameshakata tamaa kuhusu kwenda huko. Ila mama yake akaendelea. " kwakuwa umesema alishawahi kukusaidia nenda ila ujue hii saa moja, nenda kawakilishe saa tatu na nusu uwe umesharudi". Weeeeh!! Niram Nikama hausikia vizuri "mama unasema ?".lakini akisubiri jibu kutoka kwa mama yake, akihofia asije kumchanya akaghairi, alinyanyuka kwa furaha mbio mpaka kwa mama yake akamkumbatia na kumbusu. "asante sana mama nakupenda ".aliongea niram kisha akachomoka kuelekea ndani ili akaoge. "ila kama niliyokuambia, ukichelewa leo hupati tena ruhusa ".aliongea mama yake. "sawa mama sitachelewa".aliongea niram huku akaufunga mlango wa chumbani kwake. Akiwaacha mama na msichana wao mbavu hawana kwa vicheko. Maana ilikuwa kidogo niram avunje mguu kwa furaha ya kukubaliwa kwenda kwenye sherehe .
*******
Ukumbini mambo yalikuwa motomoto, watu walikuwa wameshafika,huku wengine wakiwa bado wanaingia, ama kwa hakika watu waliitikia wito. Mbali na Hapo ukumbi ulipambwa vizuri kiukweli ulivutia siyo masihara. Mr na mrs ngosha baba na mama yake vicent labda itakuwa rahisi kwa lugha hii. walikuwa bize kupokea wageni na kuwakaribisha ndani. Kikweli nao walipendeza sana, baba kwenye suti ya kisasa ya kijivujivu na mama ndani ya gauni ya bluu matata sana, yani walionekana vijana mno, ama kweli mwenye pesa sio mwenzio. Kwa mbele kidogo alionekana suma pamoja na Richad wakiwa na wapenzi wao,wakiwa wamependeza kupindukia wote wawili wakiwa kwenye suti nyeusi zilizo wakaa vyema huku na tai zao nyekundu zikizidi kuwa ng'arisha. Pembeni yao akiwa Vanessa akiwa amelipuka siyo masihara, alivalia gauni refu jekundu liliachia mpasuo mbele, chini akiwa amevaa viatu virefu vyeusi huku kichwani akitengeneza mtindo wa aina yake. Kiukweli alijua kunogaa mtoto alivutia sio kitoto. Muda huo ilikuwa saa mbili, watu karibia wote walifika hapo alikuwa anasubiriwa vicent tu.*****
Niram alikuwa amesimama juu yakioo chake, macho yote mbele akijitasmini alivyopendeza na kweli alipendeza kupitiliza wanasemaga kudamshi . Alikuwa amevalia nguo za Kihindi zinazoitwa punjab. Alivaa nusu kanzu ya pinki yenye nakshi za gold na suruali ya gold yenye ufito wa gold chini, huku viatu alikuwa amevaa vya sendo rangi ya gold. Nguo zilikuwa zimemkaa vyema na kumshika vilivyo maana suruali ilishonwa dizaini ya modo,huku blauzi ikimshika kwa juu na kumwaga kwa chini huku kimtandio cha pink na gold ukipita shingoni mwake, nywele zikimwaga mgongoni, huku Vieleni vya dhahabu pamoja na cheni nyembamba ya gold iliyopita shingoni mwake huku mkononi akiwa amevalia kisaa cha dhahabu pia maana hakupenda kuvaa bangili. Niramu alijuwa kuwaka utasema ndo ilikuwa siku yake ya harusi alivutia kupita neno lenyewe Wallah. Alichukua pafyum akajipulizia huku akiwa ana harakisha asije akachelewa. Aliwaza kwa muda na huyo akatoka chumbani kwake na kutoka sebuleni. Kumbuka kwamba maongezi aliyasikia kule supermarket, kwamba sherehe inafanyika nyumbani kwao na yeye alishawahi kufika ile siku aliyompa lifti. Kwahiyo usije ukajiuliza niram kapajuaje kwakina vicent. Alitoka mpaka sebuleni, mama yake alipomtazama alitoa macho asiamini alichokionaa. "mmh!! Mwanangu hii nguo nakumbuka tangu kukuletea kaka yako zawadi kipindi umefaulu kwenda kidato cha tano hakuwahi kuvaa imekuajee".aliuliza mama yake. "hamna mama nimeamua tu". "yani umependeza sijawahi kuona tangu umejitambua kuwa wewe ni msichana lakini leo umefunika vibaya, kuna usalama kweli huko?". Aliuliza tena mama niram, maana anamjua mwanae vizuri hata kwenye harusi hupenda kuvaa kawaida tu leo imekuajeee. Ila jibu hakulipata ."mama wacha niende niwahi kurudi".aliongea niram huku anambusu mama yake na kuanza kuondoka, "haya ufike salama mpndwa". "sawa mama".alijibu niram huku anamalizikia kutoka nje akiwaachia harufu ya manukato, akachukua gari na kuondoka zake.******
Ilishahitimu saa tatu na dakika zake, vicent alikuwa ameshaingia huku burudani zikiendelea, kulikuwa na show live kuna baadhi ya wasanii maarufu walialikwa. Vicent alikuwa chini akiwa na mpenzi wake Vanessa na marafiki zake suma na richard huku baadhi ya marafiki zao wengine waliosoma nao wakiwa wameuzulia sherehe hiyo ya aina yake. Vicent alikuwa ametinga suti kalii ya bluu bahari huku akivaa ndani shati jeupe tai nyeusi chini akipiga moka kalii nyeusi, nywele alizitengeneza kwa mtindo wa panki huku akiwa amechonga ndevu na kuziacha za wastani, zilizo mfanya azidi kupendeza. 
Vinywaji vilisaza waliokaa walikaa, waliosimama kucheza muziki walisimama ili mradi ilikuwa burudani ya kukata na shoka. Ila wakati burudani zinaendelea mara ghafla taa zote zikazimwa ukumbini na kuwa na kigiza,ila kabla hawaja patwa na mashaka wakaona stejini taa zinawaka za rangi ya gold na pinki huku zikimwekuamwekua na kufanya steji izidi kupendeza .kila mtu akashangaa kuona suprise ile, vicent akajua itakuwa wazazi wake wameamua kumfanyia. Huku wazazi wake wakijua kuwa labda vicent hatakua anajua kuhusu lile tukio linalofanyika pale na itakuwa mpango wake. Basi pale stejini baada ya kuwaka zile taa, zikazimwa na kuwaka taa za aina moja mara akatokea msichana juu ya steji aliyesimama katikati, huku anawapa Mgongo watu wale walokuwa chini ya steji. Mara ghafla miziki ikaanza kupigwa,sauti nyororo ya msichana ikasikika ikiimba ,bila kugeuza uso wake akiwa amesimama palepale ya jukwaa. "wewe ndo nikupendae" Sijawahi kupenda mwenginewe Moyo wangu unao wewe Tafadhali usiniache Njoo karibu yangu ili uniokoe" Baada ya kuanza kuimba hivyo ukumbi wote ulilipuka kelele. Maana sauti ilikuwa nzuri na tamu sana. "baby mbona bonge la suprise hili"alionge Vanessa huku akiwa anafuraha mno. Vicent alikuwa anashangaa maana hata yeye alikuwa aelewi kinachoendelea. Ila mara gafla yule msichana akageukauka huku anaendelea kuimba, weeeeeh!! Vicent macho yalimtoka miguu ilikufa ganzi baada ya kumuona niram mbele yake. Vanessa yeye akuelewa chochote alikuwa anacheza tuu nyimbo inavyotumbuizwa.niram aliimba mpaka akamaliza watu wote wakampigia makofi huku wakizidi kusadifu vizuri uzuri wake. Muda wote vicent alikuwa kimya hakujua afanye nini ila akiwa bado katika kutafakari, akasikia niram anaongea pale juu ya steji huku akiwa ameshika maiki kikamilifu. "huu wimbo ni special kwa ajili ya mwanaume nnaempenda kwa moyo wangu wote na si mwengine ni vicent, popote ulipo kama unanipenda please njoo karibu yangi".ukumbi mzima ulilipuka kelele hadi wakina suma walikuwa wanashangaa. Vicent akachopoka mbio mpaka juu ya stejii,akimwacha Vanessa ameduwaa tabasamu na furaha vyote vikiyeyuka macho yakiwa mbele, vicent alivyofika akamvuta na kumkumbatia, alafu akamnyanyua uso wake kisha akausogeza karibu yake na kusogeza midomo yake, niram hakuwa na pingamizi alijiachia wakibadilishana mate. Watu walizidi kushangilia maana waliona ni moja ya suprise kwa wageni kama wao. Ila wazazi wake walikuwa katika mshtuko maana walijua vicent yuko na Vanessa sasa imekuwaje. Ila mara gafla baba vicent akamwona vanaessa anatokea jikoni huku anaelekea juu ya steji.akamshtua mkewe amuangalie mama vicent akatupa macho kumuangalia ila kuna kitu akaona. "baba vicent nenda kamuwahi ameshika kisu".alibwatunga mama vicent, pasipo kujiuliza baba vicent akachomoka mbio kumuwahi vanesa asije kufanya balaa, ila vanesa alikuwa amemuacha mbali sana maana alikuwa anatembea haraka haraka. Pale stejini vicent na niram wakaachiana ,vicent akamtazama tena usoni na kumtakia. "nakupenda sana niram". "nakupenda pia na sitaki kukukosa tena".alijibu niram baada ya hapo wakakumbatiana tena ila vicent akiwa amemkumbatia niram,mbele yake akamuona Vanessa anakuja mkuku kwa umbali akifuatiwa na baba yake, lakini vicent hakuelewa kuna nini maana alimuona kama baba yake anaongea kitu ila akusikika kutokana na makelele, kutahamaki Vanessa akachomoa kisu kakinyanyua juu tayari kumchoma nacho niram ila vicent akamgeuza niram kwa kasi ya ajabu kikamuingia yeye tumboni, mpaka baba yake anafika vicent tayari alikuwa ameshadondoka chini. Vanessa alivurugwa akutegemea ila gafla akakimbia na akuna aliemjali kila mtu alikuwa anamkimbilia vicent. Niramu alikuwa amemkumbalia vicent huku nguo zake zikiwa zimechafuka damu analia kama mtoto,vicent alikuwa anapumua kwa shida mno, lakini akijitahidi akamvuta niram na kumnong'oneza ."nakupenda "kisha akatulia kimya, niram alipigaa kelele za ajabu huku mishipa ya kijani ikionekana hapohapo nayeye akadondoka. Itaendelea ...........

Where do you want to donate?

Traktir Kopi
Bank BCA - An. Asep Saepul Anwar/ Rek - 648xxxx
Treat the creator to coffee by giving a small donation. click the arrow icon above

Chapisha Maoni

Copyright ©BongoLife - All rights reserved.

Redesign by bloggun.xyz
Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
More Details