CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu) SEHEMU YA 11

CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu)

MTUNZI: Minnah De Embaccas

SEHEMU YA KUMI NA MOJA (11)

Whatsapp :0656282898

ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI: aliongea niram huku ananyanyuka na kuondoka. "niram".alijaribu kuita vicent ila hakujibiwa. Niram alikazana mpaka alipofika kwenye gari lake akapanda gari akawaasha na kuondoka. Kwakweli vicent alichoka mtoto wa kiume alitokwa na chozi la maumivu hakutegema, hakuamini kama yametokea yale. Alichukua lesso akafuta machozi, alisimama na kuanza kuondoka ila ghafla, endelea......
Ila ghafla akawa kama ameona kitu kwenye meza ile aliyo kaa niram. Alipo angalia vizuri niram alikuwa amesahau miwani yake juu ya meza.vicent aliichukua akaitazama kwa muda kisha akaichukua akianza kuondoka. Watu waliokuwepo pale walibaki kumshangaa hawakujua nini kilichopelekea mpaka yule msichana wa Kihindi kuondoka, ila walihisi kutakuwa na kitu kati yao kilichopelekea yule dada kuondoka. Basi vicent akaanza kujiongea taratibu kuelekea nje ya eneo lile, huku wale waliokuwa wanamtazama waliamua kufanya mambo yao. Vicent alifika sehemu alipopaki gari lake akaliwasha kwa spidi kaliii huku akiacha vumbi huku nyuma.
*****
Niram alifika nyumbani kwao, akapaki gari akashuka moja kwa moja mpaka chumbani kwake. Alimkuta mama yake sebuleni lakini kama vile hakumuona alimpita vuuup hata salam akuitoa. Kiukweli ile hali mama yake alishangaa hakujua kimemkuta nini binti yake mpaka kupelekea kuwa katika hali hileee. "mmmh! Alipotoka huko kwema kweli? ".alijikuta anajiuliza maswali mwenyewe na jibu asilipate. Alichoamua ni kunyanyuka moja kwa moja akaelekea kwenye chumba cha binti yake na kuanza kugonga mlango lakini akuitikiwa .mama niram akaamua afungue na kuingia alimkuta niram analia shuti uso umekuwa mwekundu. Ikabidi mama yake apite ndani na akakaa pembeni yake huku akimtazama kwa huruma japo hakujua ni nini kilicho msibu mwanae. "vipi binti yangu kuna tatizo gani huko ulipotoka?". Niram hakujibu lile swali zaidi aliendelea kulia kilio cha kwikwi akionyesha Zahiri hilo jambo limemuumiza kupita kiasi. Mama niram alipoona kuwa siyo rahisi kama alivyotegemea kwa sababu alimjua mwanae akiwa na hasira huwa awezi kuzungumza. Alimvuta kwake na kumlaza mapajani mwake huku akimpigapiga mgongoni akimbembeleza mpaka alivyo muona amekuwa sawa akaanza kumuuliza. "haya niambie mama kuna nini huko mbona umerudi hivyo? ". Niram alinyanyuka mapajani mwa mama yake akafuta machozi na kuanza kumwambia. "mama hali ya mgonjwa haipo vizuri, anapumulia mashine kikweli anatia simanzi ".aliongea niram kwa kumuangalia unaweza kusema kweli hicho ndicho kinacho mliza ila kikweli ukweli tunaujua sie. Mama niram akaamini moja kwa moja kwamba ile ndo sababu iliyopelekea mwanae kuwa vile kwasababu anamjua niram ni mtu mwenye huruma sana kwasababu hata ndugu yake yoyote akiumwa niram ni mwepesi sana kulia. "pole sana mwanangu tumuombee kwa Mungu arudi kwenye uzima". "amiiiin mama".alijibu niram na mara baada ya kumuona mwanae amerudi kwenye hali ya kawaida akamwacha apumzike yeye akaenda zake nje kuenda kumsaidia msichana wake waka kazi kuandaa chakula cha usiku. Niramu baada ya kutoka mama yake alianza kulia upya maana alijikuta kama kuna kitu chenye ncha kali kinauchoma moyo wake kiukweli aliumia sana. "siyo kama sikupendi vicent, nakupenda tena sana lakini unafikiri itakuwaje tumetofautiana dini hata jamii zetu ni tofauti wazazi wangu hawatanielewa nisamehe sana ila sina cha kufanya".alijikuta anatamka maneno hayo bila kujijua huku akilala na kujikunyata machozi yakizidi kulowanisha shuka. Baada ya kulia kwa muda mrefu niram akapitiwa na usingi akalala hapohapo. 
********
Vicent muda wote alikuwa ndani kwake chumbani amejifungia.na alishatoa maagizo kwa msichana wa kazi kuwa asiende kumgongea wakati wa chakula ajisiikii vizuri anapumnzika. Basi alikuwa amekaa kwenye kochi lililokuwa ndani kwake alikuwa ni mtu mwenye mawazo sana. Hakutegemea kuwa itakuwa vile kiukweli aliumia sana. " madhari kaamua iwe hivyo basi sawa,hata misemo inasema usifosi kosa kuwa pata kila kitu kinakwenda na riziki acha aende ntatulia na Vanessa labda ndo fungu langu".alijiwazia vicent akachukua simu yake akaitazama namba ya niram kwa muda kisha akazifuta na kumblock kotekote. "kwaheri niram tutaonana Mungu akipenda".alijisemea kwa sauti vicent akaiweka simu pembeni na kulala. Aikupita muda mrefu simu yake ikaanza kuita, akaamka na alipoangalia ni nani anaepiga akamkuta vanessa. "naam mkewangu ".vanessa aliposikia ameitwa hivyo, moyo ulimlipuka kwa furaha, akuamini hakuweza na akutegemea maana ilikuwa muda mrefu ajaitwa hilo jina. "poa tu baby nimekumisi nikaona nikupigie".aliongea Vanessa kwa uwazi kabisa ilionyesha alikuwa na furaha isiyo kifani. "nimekumisi pia mke yani ndo nilikuwa nawaza kukupigia nawewe ndo unapiga". "mmmh!! Vicent kwa uongo sikuwezi".aliongea Vanessa kwa sauti fulani hivi ya madeko. "yaah! Ni kweli mama yangu siwezi kukudanganya".aliongea vicent kwa sauti isiyozidi kumtekenya Vanessa na kujiona hakuna kama yeye kwenye hii dunia. "aah sawa mpenzi mi nalala nilikuwa nataka kusikia sauti yako tu". "Oky honey ulale salama i love you"..aliongea vicent na vanesa akamjibu "love you too".basi waliagana na simu ikakatwa kiukweli Vanessa alipotoka pale alifurahi sana hakutegemea alirukaruka kwa furaha ndani kwani kwake huku akirusharusha mito pakawa shagarabagala mule ndani. "nilikuwa namuhisi vibaya mpenzi wangu kumbe fikira zangu zilikuwa za uongo vicent wewe ni wangu tu tena peke yanguu". Aliongea kwa furaha mpaka mdogo wake alipomgongea mlango akimuomba amfungulie mlango. "dada nifungulie bwana ".ilikuwa sauti ya juliana. Aliposikia sauti ya mdogo wake akatandika kitanda haraka haraka akaweka mito vizuri pakawa kama mwanzo kisha akaenda kufungua. "dada muda wote huo unajifungia kama unalala pekee yako".alilalamika juliana huku anaingia ndani. "mmh na wewe nilipitiwa na usingizi".alijitetea Vanessa nae anaingia ndani bila kuufunga mlango kwasababu bado mdogo wake mmoja Alikuwa ajaingia. "mmh!! Wakati nilisikia unapiga kelele humu".aliongea juliana huku anazivua nguo zake na kuvaa za kulalia. "saa ngapi labda itakuwa nyumba za jirani siyo mimi".alijitetea Banissa. Jualiana akibaki kumuangalia asimjibu kitu akapanda zake kitandani na aikupita muda mrefu akapitiwa na usingizi. Vanessa nae akachukua shuka huku akiwa anatabasamu akajifunika akalala. 
********
Niram kila analolifanya alifanyiki kila anavyojitahidi kuutafuta usingizi aukuja kirahisi. Aliamua anyanyuke akachukua vitabu na kuanza kujisomea na muda wote huo akuona simu ya vicent kumpigia wala msg kutumiwa. Alijaribu kusoma nako wapi hakuweza alizidi kuvurugwa akaanza kujutia Kwa alichokifanya maana alijua fika ule ulikuwa kama uzalilishaji ajikuta anaanza kulia tena. "hato nisamehe mimi nilikuacha Kwa aibu kwakweli naomba kama masaa yarudi nyuma nimwambie kuwa nampenda pia na sitowahofia wazazi wala chochote kile ooh Mungu wangu ntafanya nini?".aliongea kwa manung'uniko niram kiukweli alitia huruma sana. Alikaa chini kwa muda mrefu akitafakari mara mlango ukafunguliwa akaja mama yake na sahani ya chakula na kumwambia mwanae ale. "kiache hapo mama ntakila maana nataka nijisomee kidogo ".aliongea niram huku anajifanya kuvuta vile vitabu. "sawa usisahau kukila hicho chakula mi naenda zangu kulala".aliongea mama yake huku anaenda zake
Niram alimuangalia mama yake alivyomuona ametoka tu akaufunga mlango na kurudi kukaa kwenye kitanda chake.alijifikiria kwa muda akaamua bora achukue simu ampigie ili amuombe msamaha na kumwambia kuwa hata yeye alikuwa akimpenda, alitafuta jina la vicent akalibofya na kuisiliza jibu alipokutana nalo lilimkatisha tamaa alikuwa apatikani. Akamtext whatsapp akaona kimya alivyo angalia vizuri akakuta vicent amemblock "Oooh!! Mungu wangu vicent usinifanyie hivyo".alijikuta anaropoka niram huku mikono kaweka kichwani simu imemdondoka hata kuijali akuijali alivyoangalia pembeni akaona..... Itaendelea

Where do you want to donate?

Traktir Kopi
Bank BCA - An. Asep Saepul Anwar/ Rek - 648xxxx
Treat the creator to coffee by giving a small donation. click the arrow icon above

Chapisha Maoni

Copyright ©BongoLife - All rights reserved.

Redesign by bloggun.xyz
Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
More Details