CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu) SEHEMU YA 13

CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu)

MTUNZI: Minnah De Embaccas

SEHEMU YA KUMI NA TATU (13)

Whatsapp :0656282898

ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA MBILI : gafla akakimbia na akuna aliemjali kila mtu alikuwa anamkimbilia vicent. Niramu alikuwa amemkumbalia vicent huku nguo zake zikiwa zimechafuka damu analia kama mtoto,vicent alikuwa anapumua kwa shida mno, lakini akijitahidi akamvuta niram na kumnong'oneza ."nakupenda "kisha akatulia kimya, niram alipigaa kelele za ajabu huku mishipa ya kijani ikionekana hapohapo nayeye akadondoka.ENDELEA........
Hapo hapo na yeye akadondoka chini na kupoteza fahamu, pale ukumbini kila kitu kili haribika,hakuna aliyekuwa na hamu ya sherehe tena. Mama yake vicent alikuwa hoi akipepewa maana presha ilikuwa juu sana. Mara baada ya muda kidogo ikaja gari ya kubebea wagonjwa mahututi, pamoja na maaskari waliokuja kuchunguza eneo la tukio. Askari walifika pale wakafanya kazi yao, na walipomaliza wakachukua wagonjwa na kuwaingiza kwenye gari lililokuja kwa ajili ya kubebea wagonjwa (ambulance). Ilikuwa ni kitendo cha haraka bila kuchelewa, vicent na niram wakiwa awajitambui,huku vicent akiwa anatoka damu nyingi sana.baba na mama yake waliingia kwenye gari hilo la wagonjwa japo mama yake na vicent hakuwa kwenye hali nzuri, lakini aling'ang'ania kwenda, na wao wakaamua kumchukua. 
Sasa turudi nyuma kidogo ili wote tupate kuelewa niram,ilikuwaje mpaka akapata nafasi ya kuimba kwenye sherehe ya vicent. Ilikuwa hivi niram alivyofika pale ukumbini alidhuiliwa kwakuwa hakuwa na kadi ya mualiko. Lakini niram alisisitiza kuwa alipewa hivyo ilimpotea,lakini walinzi hawakuamini kwakuwa walishaambiwa kuwa wasimruhusu mtu asiye na kadi kuingia ukumbini. Ila niram akawaambia kuwa alikuwa nayo ila ilimpotea na kuwaaminisha aliwaonyesha namba ya vicent na chatting zote walizokuwa wanachat kwa kawaida hadi whatsapp. Wale walinzi walipooanisha namba za mule na za kwenye kadi wakakubali na kumruhusu aingie. Ilikuwa ni furaha ya ushindi kwa niram, akaingia ndani ya ukumbi watu walikuwa wengi sana ila hakajipenyekapenyeka mpaka akamfikia dj na kumuambia kuhusu suprise yake mwanzo ilikuwa ngumu ila niram alimshawishi na kwakuwa alikuja na cd yake, basi mipango ikafanywa akaitwa mc akapewa mchongo huku niram akiwa amewapa kiasi kikubwa cha pesa basi kila kitu kikawa sawa.unaambiwa kwenye Uzia penyeza rupia. Basi ndivyo ilivyokuwa mpaka niram akaingia ukumbini, laiti wangejua wasingeruhusu jambo hilo kufanyika, ila ningejua huja mwisho wa safari. 
*******
Walifika hospitali kubwa ya Muhimbili, ilikuwa mida ya saa tano usiku, manesi walikuja mkuku kuwachukua, huku niram akiwa anapelekwa hodi ya kawaida, huku vicent akiwa amepelekwa hodi ya watu mahututi ni (I. C. U) akiwa ametokwa na damu nyingi mno. Mama vicent muda wote alikuwa analia kama mtoto mdogo, mpaka sauti ilishaanza kukauka, muda wote baba vicent alikuwa amekaa kwenye benji akimtuliza mke wake. Huku (I. C. U) madaktari wakiendelea kupigania uhai wa vicent kuhakikisha kuwa anakuwa sawa. Upande wa wodi ya kawaida niram alitundikiwa dripu ili kufanya arudishe fahamu kwa haraka. "mmewangu, vicent wangu mimi baba yangu mimi uwiiiiiiiiiiiih!! "ilikuwa ni sauti ya mama vicent, alikuwa hoi taabani kwa kulia bila kunyamaza, japo baadhi ya ndugu walikuwepo pale kuwafariji ila hakuweza kunyamaza kiukweli alitia huruma, hama kweli uchungu wa mwana aujuaye mzazi. "jitahidi mkewangu mtoto atapona tumuombee tu".ilikuwa sauti ya baba yake vicent ila muda wote alikuwa analilia pembeni, ili kumfanya mkewe asizidi kuchanganyikiwa japo nayeye alikuwa anatamani apige hata kelele kwa uchungu aliokuwa anausikia ulikuwa aulezeki. Suma na richard walikuwa wamesimama pale nje ya wodi,hatua chache na wazazi wa vicent wakiwa wanatokwa na machozi yasiyo zuilika. Yani kila mtu alikuwa yupo hapo hakuwa sawa kabisa. 
*********
Mama niram alikuwa bado ajalala ,mpaka muda huo wa saa sita na robo usiku, alikuwa peke yake kwenye sebule msichana alikuwa ameshalala kiufupi alikuwa ameshaanza kupata wasiwasi ."mmmh huyu mtoto mbona anataka kuniua na presha jamani ".alisemea mama niram huku anaivuta miguu yake na kuiweka sawa kwenye kochi alilokalia akiwa kama anataka kujilaza. Ila mara gafla alisikia simu yake inaita, na alipotazama akaona anae mpigia ni namba tu bila jina ilikuwa namba ngeni. "mmh nani huyuu? Mbona usiku kulikoni ".alijiuliza ila hakutaka kupoteza muda sana akapokea na kuiweka sikioni. "hellow" alisema mama niram, ila haikusika upande wa pili, mara mama Niram akaguta kelele na kuanza kulia kwanguvu. "mwananguuuuu mieeeeeee mama weweeeeee".alikuwa analia mama niram, ni kelele zilizo mshtua msichana wa kazi na mlinzi, ilibidi msichana aje mbio akamwona bosi wake anagalagala chini huku analia,akaona bora akanfungulie mlinzi ili kusudi wasaidiane. Basi mlinzi aliingia wakamtuliza na kumuuliza kulikoni. "jamani nimepigiwa simu niram amepoteza fahamu na yupo Muhimbili hata sijaoji vizuri nikawa nimepatwa na mshtuko ,jamani mwananguu".aliongea huku akizidi kulia, ilibidi msichana aingie ndani na kumtolea dela avae, mlinzi alienda kumsubiri nje. Baada ya hapo msichana alibaki nyumbani huku mlinzi akimuendesha bosi wake maana Hakuwa hata na nguvu, muda wote alikuwa analia tu. Walitoka speed mpaka Muhimbili, na waliwahi kufika kutokana na kuwa hakukuwa na foleni usiku huo******
Tuje upande wa kule ilipotokea simu aliyopigiwa mama niram, ilikuwa hivi baada ya niram kupanda pale juu ya steji, aliacha simu kwa dj na yeye kwenda kutumbuiza pale juu. Na hata lilipotokea liletukio bado simu ilikuwa mikononi mwa dj,kutokana na kughafilika hakuwa na wazo la kupiga simu muda ule lilipo tokea lile tukio. Ila baada ya muda ndo alipogundua kuwa ana simu ya yule msichana wa Kihindi, akiangalia labda kama anaweza kufanya chochote kitu ila kwa bahati nzuri alikuta simu aina passwod akaona hiyo ni neema kubwa, akaangalia namba mara akaiona iliyoseviwa mama,basi hapohapo akaanza kupiga lakini simu aikuwa na salio,ndipo alipohamisha namba kwake na kumpigia mama yake niram ili kumjulisha hali halisi iliyomkuta mtoto wake. 
******
Matibabu yaliendelea na bahati nzuri vicent alitoka kwenye danger. Alipelekwa hodi ya kawaida huku akiwa amewekewa drip ya damu kwa maana alitokwa na damu nyingi mno.japo bado fahamu zilikuwa bado azijamrudia lakini alikuwa Ameshafanyiwa upasuaji na alikuwa ajachomwa sehemu mbaya na kile kisu ndo maana hata upasuaji ilikuwa imefanyika kwa uharaka. Kidogo baba mama, marafiki zake na ndugu zake pia vicent, walikuwa wamepata matumaini baada ya kumuona vicent kapelekwa wodi ya kawaida japo fahamu bado aija mrudia. "dokta lakini atapona mtoto wangu?".ilikuwa ni sauti ya mama vicent baada ya kumuona dokta akitoka chumba cha mwanae, akiwa anatoka kumtundikia drip. "usijali mama atakuwa sawa".alijibu daktari. "vipi na kuhusu yule binti anaendeleaje ?".aliuliza baba vicent alikuwa ana muulizia niram. "mmh!! Tatizo lake siyo kubwa ila japo hii ni dripu ya tatu tuliyo mwekea ila bado ajarudiwa na fahamu".alijibu daktar kwa umakini na hali ya sitofahamu maana hali ya niram ilikuwa aijatengamaa. "mmmh".aliguna baba vicent, na kumchukua mkewe wakaenda kukaa kwenye benji,na daktari akawa anaondoka kuelekea ofisini kwake ila gafla akaingia mama yake niram akifuatiwa na mlinzi wake nyuma. Alikuja mkuku huku anahema kwa nguvu,alimuwahi na kumshika dokta kabla ajaingia kwenye ofisi yake. "dokta mwanangu yupo wapi? Niambie au amekufa niambie".aliongea mama niram huku anamkwida dokta kwa nguvu akimtikisatikisa, kiukweli mama niram alikuwa ni kama mtu aliyechanganyikiwa. Baba vicent pamoja na mkewe wakiwemo na wakina richard, walisogea mpaka pale alipokuwa daktari na mama yake niram ,ili kuenda kumtuliza. Hata daktari hakuwa na jibu alibaki akiduwaa na kukosa cha kumjibu. Ila wale wote walimjua kuwa ndo mzazi wake niram maana walikuwa wanafanana sana na niram. "mama tulia mwanao yuko salama anaendelea na matibabu".alijibu dokta baada ya kusaidiwa kutolewa kwenye mikono ya mama niram. "kimempata nini mwanangu jamani".aliongea huku analia akielekea alipokuwa anapelekwa na wazazi wa vicent, wakamweka kwenye benji na wao wakakaa ili waanze kumueleza. Dokta baada ya kuona mambo yamekuwa sawa akafungua mlango wa ofisi yake ili aingie, mara akamsikia nesi anakuja mbiombio huku anamwita "doctorrrrrrrrrrr".................. Itaendelea,

Where do you want to donate?

Traktir Kopi
Bank BCA - An. Asep Saepul Anwar/ Rek - 648xxxx
Treat the creator to coffee by giving a small donation. click the arrow icon above

Chapisha Maoni

Copyright ©BongoLife - All rights reserved.

Redesign by bloggun.xyz
Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
More Details