CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu) SEHEMU YA SABA (07).

CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu)
 
MTUNZI: Minnah De Embaccas

Whatsapp :0656282898

SEHEMU YA SABA (07)

ILIPOISHIA SEHEMU YA SITA: Niram alikuwa chumbani kwake akijisomea, wakati huo alikuwa ameshakula, alikuwa kitandani miguu kuegemeza ukutani, muda wote alikuwa mtu mwenye tabasamu usoni, kilicho mfurahisha akijulikani
Mara ghafla simu ikaanza kuita. endelea........
Mara gafla akaona simu inaanza kuita. Niram akaangalia mpigaji, akaona namba ngeni. " mmh! Atakuwa Nani huyu?".alijiuliza niram, alitafakari Sana maana sikawaida kupigiwa na namba ngeni, baada ya kutafakari kwa muda.akaamua kupokea. "hellow".aliitika niram. "hallow Niram huko poa?, Vicent hapa". Ilisikika sauti upande wa pili."oooh! Vicent nashukuru mungu niko poa sijui wewe ulifika salama? ".alijibu niram nakupachika swali. "nilifika salama niram hofu ilikuwa kwako".alisema vicent. "namimi nashukuru mungu nimefika salama".alijibu niram kwa sauti nyororo kabisa. 
******
Vanessa alikuwa ndani kwake akaona mbona muda unaenda sana,na ajaona msg wala simu kupigwa kutoka kwa vicent. Alikaa akasubiri na kusubiri weeeeh lakini ikawa kimya. "mmmh!! Ina maana itakuwa ajarudi bado huko alipoenda"alijisemea mwenyewe, akaona muda unaenda lakini simu aipigwi. "mmh ngoja nipige"aliamua apige yeye, akachukua simu yake na kuipiga. Jibu alilokutana nalo ni NAMBA UNAYOPIGA INATUMIKA KWA SASA.. "mmmh saa tano hii au ndo amerudi hivyo anaongea na wenzie kuwa julisha kuwa amerudi?".alijiuliza jibu akakubaliana kuwa anawasiliana na rafiki zake. 

******
Huku vicent akiwa anaongea, akaona kama kuna mlio wa simu nyengine kuingia akaiangalia , alipoona mpigaji kuwa ni Vanessa akaendelea kuongea. Simu iliita mpka ikakata. Waliongea mengi na baadae niram akaaga kuwa anahitaji kupumzika. Basi waliagana na simu ikakatwa. 
Baada ya hapo alipiga simu kwa Vanessa,huku Akiwa ameshaupanga uongo wa kumwambia. "hellow baby mbona kimya, na napiga unatumika?".aliongea vanessa mara baada ya kupokea simu. "aaah amna nilikuwa naongea na mzee maana mchana,hakuwa na nafasi ndo kunitafuta sasahivi".alijibu vicent kwa ujasiri wa hali ya juu,bila kubabaisha maneno. "oooh kumbe haya niambie mizunguko ilikuwaje? ".Aliuliza Vanessa huku alibadili mikao ya kila aina Hapo kitandani. "ilikuwa poa sema nimechoka sana".alijibu vicent huku akijifanya anapiga mihayo. "oooh basi pumnzika baba angu tutaongea kesho".aliongea Vanessa kwasauti fulani hivi ya madeko. "sawa mama ntakuchek kesho ulale salama"alimaliza kuongea vicent akakata simu. Alienda moja kwa moja bafuni akaoga, maana choo kilikuwa ndani kwake humohumo. Alipomaliza alitoka sebleni muda ulikuwa umeenea sana ila alikuwa bado ajala, alikuta msichana ameshaenda kulala,aliwasha taa ya sebuleni akachukua sahani jikoni nakuenda kula chakula. Mara ghafla akasikia mlango unafunguliwa alikuwa mama yake, "yani wewe Bwana mi nilivyorudi nikaambiwa upo ndani nikajua ushakula".aliongea mama yake vicent,huku anavuta kiti pale sehemu ya kulia chakula akakaa. "hapana mama uwezi amini yani nilipitiwa na usingizi nikalala ndo nimeshtuka sasa hivi".aliongopa vicent, aisee huyu jamaa hatari."ooooh pole baba ni uchovu tu huo"aliongea kwa huruma mama yake. "asante mama".alijibu vicent huku anafakamia wali kwa maini. Basi waliongea mengi mama mtu alinyanyuka, na kuenda kulala. "ukimaliza usisahau kuzima taa baba".aliongea mama yake. "sawa mama ntaizima".vicent alikula akashushia juisi, akaelekea kwenye swichi akazima taa na kuenda kulala. 

*******
Pilikapilika zilikuwa zinaendelea, katika nyumba ya kina niram.ilikuwa Jumapili kulikuwa na ugeni mkubwa kwao, kuna ndugu zao walikuja.basi yalipikwa masontojoo siyo ya kawaida. Zilisagwa juisi za matunda basi ilikuwa tafrani. Niram akutulia alikuwa bize vibaya. "niram ebu kuongezeae chumvi kwenye biriani kule".ilikuwa sauti ya mama yake. "sawa mama".alijibu huku anaacha alichokuwa anafanya na kwenda kuweka chumvi kwenye chakula. Kila kitu kilikuwa sawa sasa niram alikuwa chumbani anajiandaa akaoge. 
********
Suma alipoona ajapigiwa jana, akaona isiwe kesi ngoja amchek yeye maana umbea ulikuwa unamuwasha mtoto wa kiume huyu. Akukubali kitu kimpite hivihivi,yani alikuwa tofauti na richard mwenzie hakuwa mpenda kufuatilia yasiyo muhusu. Basi aliweka vocha akampigia "oyaaa mwanangu unayumba"haliongea suma ."hamna nilichoka sana yani uwezi amini ".alijibu vicent. "eeeh ilikuwaje jana na yule mtoto mzuri?".aliongea suma huku akitegesha masikio vizuri kupata udaku "hahhhhah suma eeh nna kazi kama unataka kuhusu hiyo stori ntakupigia baadae " "ok poa basi usisahau ".alijibu suma huku anakata simu. Ila suma akakumbuka kitu ayaaaaaah!! Daaah!!.Nimesahau kumuuliza Kitu, yeye na haraka zake mpaka nimesahau".aliongea suma huku anamlaumu vicent,kwa uamuzi wa kukata simu haraka. "anyway nitamchek baadae".aliongea suma, mara kisimu chake kikaanza kuita."duuuh huyu somoe ana mpya gani nae mi leo nnampango wa kuonana na hadijaa".alijiseme suma kimoyomoyo ,huku anaangalia ile simu bila kuipokea. Labda niwafafanulie vijitabia vya huyu ismail au kwa ufupi ndo unaweza kumuita suma. Yani suma yupo tofauti na wenzake, suma kwanza ni mwingi wa habari,anapenda kujua mambo ya watu ni mwongeaji mno kuliko wenzake.ajatulia hata kidogo isimpitie sketi mbele yake lazima amfate tu, ila richard na vicent wapo tofauti sana na yeye, richard ana mahusiano na binti mmoja anasoma, shule tofauti na yao. Na ni huyohuyo tu ndo yupo nae. Lakini suma weeeeeeh!! Mwiko mkubwa tena uchuro, kutulia na mwanamke mmoja. Basi baada ya simu kukata akaizima na kuendelea na mambo mengine. 
*******
Ilikuwa ni mida ya jioni. Wageni wameshaondoka, nyumbani kwa kina niram. Na mama yake kama unavyomjua mtu wa pilikapilika usiseme, alikuwa ameshaenda kuzurura muda mrefu. Aaaaah ahhh!!,sijui muhindi gani huyu mwenye tabia za Kiswahili.ok tuachane nae tuendelee. Basi niram alikuwa amekaa sebuleni peke yake, maana mdada wa kazi hupendelea kukaa ndani kwake kama kazi ameshazimaliza. Basi alijikuta mpweke sana na alijikuta anatamani, kuongea na vicent,ili apate kampani na kupoteza muda kidogo. Hata sijui ni kwanini alimuwaza vicent kuwa ndio mtu pekee wa kumtoa upweke. Hata mimi sijui,ila tutajua hivi karibuni. Basi aliingalia simu kwa muda nakujifikiria ampigie au atulie asimpigie. Basi nafsi ya niram ikawa inashindana,moja inamwambia piga nyengine, inamwambia usipige ila akiwa katika mgongano wa kutoa maamuzi nini afanye, gafla akaona kitu moyo ukapiga paaaaah!!! .alishindwa kuamini alichokiita. Itaendelea....

Where do you want to donate?

Traktir Kopi
Bank BCA - An. Asep Saepul Anwar/ Rek - 648xxxx
Treat the creator to coffee by giving a small donation. click the arrow icon above

Chapisha Maoni

Copyright ©BongoLife - All rights reserved.

Redesign by bloggun.xyz
Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
More Details