CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu) SEHEMU YA NNE (04)

CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu)
 
MTUNZI: Minnah De Embaccas

 Whatsapp :0656282898

 SEHEMU YA NNE (04)

ILIPOISHIA SEHEMU YA TATU: "aaah! basi kausheni vipi ile story ya asubuh nimalizie basi mwana".aliongea Richard huku anajiweka sawa kusikiliza. Vilifwata vicheko hatari. "kumbe na wewe shilawadu" aliongea suma baada ya kumaliza kucheka. Basi story zikaanza upyaa, visent akampa fully data. Richard Akuwa na la kuchangia zaidi ya kumtia moyo na kumwambia akaze buti. mara wakasikia... endelea.......
mara wakasikia, kama kuna vishindo vinakuja mahali walipo wao .ilibidi wakatishe story yao.nakuangalia mbele palipotokea,sauti ya viatu."mmmmh!!", alishusha pumnzi vicent baada ya kumuona mtu huyo aliyekuwa anakuja usawa waliokuwepo wao. Hakuwa mwengine bali ni vanessa, vanessa alizidi kuiongea taratibu kuja mahali pale, walipokuwepo wakina vicent.hatimae alifika."mambo zenu". Aliwasabahi huku akisubiri atajibiwa kwa hali gani salamu yake."nzuri vp vanessa"alijibu suma, mara kabla ajamaliza kuitikia suma, alidakia richard pia."tuambie shemela wa ukweli".kauli hii ili mchukiza, sana vicent alijikuta anamkata jicho moja kali rafiki yake huyo.ila vanessa alipotezea japo vicent,hakujibu salamu yake. "mi niko poa sana samahanini shemeji zangu nilikuwa naomba mnipishe kidogo nna mazungumzo na vicent".aliongea vanesa, huku akiwaangalia shemeji zake hao kwa zamu."ooh!!usijali mama suma eeh tuwapishe wapendanao".aliongea tena richard safari hii huku anatabasamu tabasamu la kichokozi,maana alijua ni jinsi gani anamkera rafiki yake." twenzetu mwanangu uwanja wenu jamani".aliongea suma huku ananyakua kibegi, chake kilicho kuwa pembeni yake, amesimama na kuanza kuondoka,wakati huo richard alikuwa ameshatanguli mbele." oyaa wanangu msifike mbali mnisubiri maana sitachukua mda mwingi hapa".aliongea vicent huku akiwa bize anatazama walipo kuwa wana tokomea wenzie. " poa".walijibu wote kwa pamojaa na kuendelea kutokomea mbele. "nakusikiliza unaweza kuongea" aliongea vicent bila kupepesa macho, akiwa mkavu kabisa." vincent kwani una nini mbona sikuelewi baba"aliongea vannesa huku anakaa pembeni ya vincent. Ila akupata jibu toka upande wapili."vincent si naongea na wewe au kuna kitu nimekukosea niambie ili nijue nikuombe radhi baba,nakupenda sitaki tukosane".aliongea vanesa kwa huzuni huku machozi yakiwa yanalengalenga kwenye macho yake. "sikia vanessa naomba usipoteza muda wako kwa ajili yangu focus katika masomo ujui kuwa tuna karibia mitihani ya kuhitimu kidato cha Sita ".alisema visent bila alama ya uoga,usoni kwake."najua baba lakini hiyo siyo sababu ya kufanya uwe serious ni kuelewana tu" alilalama vanessa huku akijisigeza karibu na vicent."oky basi ndo hivyo vanessa tuzingatie masomo now mapenzi yasimame kwanza".alimaliza vicent huku akijifuta vumbi, kwenye makalio tayari kwakuondoka. "vicent ntawezaje kukuchunia siwezi ntajitahidi nisome kwa bidii ila tusisitishe uhusiano wetu nakupenda sana". "vanessa tuelewane basi au nimefanya kosa kukusikiliza hapa?". Aliuliza vicent,pasipo kusubiri jibu akaanza,kuondoka.ila vanessa alimdaka mkono,na kumvuta asiondoke.daaaaah!! Lilikuwa kosa kubwa maana alisukumwa,akadondoka kama mzigo wa kuni pwaaaaaaah!!.aisee!! Vanessa aliumia akaanza kulia, maana alijiona kama mtu asiekuwa na thamani tena, aliumia kupita kiasi. Kitendo kile, kilimfanya vicent aingiwe na huruma, akaghairisha alipokuwa anakwenda, maana alijiona ana hatia sana. "nyanyuka mpenzi sikuzamilia kufanya hivyo nisamehe mama ". Alisema vicent huku akiinama, kumnyanyua vanessa na kwa bahati nzuri, hakuna alieliona tukio lile. "pole mama nisamehe sana". Alisisitiza vicent akionyeshwa kuchukizwa, na tukio alilolifanya." usijali vicent najua aikuwa kusudio lako kuna vitu haviko sawa kwako". Alijibu vanessa huku anajifuta vumbi, akisaidiwa na vicent. Baada ya hapo vicent alimchukua na kumkalisha chini. " vanessa siyo kama sikupendi laah hasha!! Nakupenda ila nielewe unatakiwa tusome kwanza tukimaliza mitihani tutaendelea, nafanya haya kwaajili yetu mama".aliongea vicent,siyo kama alimaanisha ila aliona si busara, kumuhukumu mtu kisa kampenda ni dhambi kubwa sana. " sawa ila niahidi tutakuwa tuna ongea hata mara moja moja, kwani bila kusikia sauti yako au kukuona sitaweza kusoma". Aliongea kwa kudeka, huku akijiegemeza kwa vicent. " sawa mama itakuwa hivyo ila naona muda unatutupa mkono, sitaki kuwachosha wenzangu wananisubiri". Alisema vicent huku akisimama tayari kwa kuondoka. "oky bby tutawasiliana ukifika".alisema Vanessa huku akiachia, busu matata shavuni mwa vicent. Basi waliagana na vicent akawafata washkaji zake, safari ikaanza..******
Nyumbani kwa kina niramu, palipoa alifika moja kwa moja mpk nyumbani kwao, akamsalimia dada wa kazi " da anna mamy yuko wapi?" aliuliza huku ana jibwaga juu ya kochi, begi akilitupia juu ya meza kubwa ya kioo, " ametoka kaniaga anaenda supermarket kununua bidhaa zimepungua".alijibu anna msichana wao wa kazi.niramu akajizoazoa kivivu, akaliokota begi lake, akaelekea chumbani kwake. Anna aliondoka kuendelea na shughuli zake.*******
Vanessa alifika kwao, alikuwa amechoka, alifika akamkuta baba yake, ametulia kwenye kochi,akisoma gazeti. Nyumba yao ilikuwa, kubwa kiasi yenye uzuri wa kawaida.baba yake alikuwa daktari hospitali ya muhimbili, mama yake alikuwa mwalimu wa shule ya msingi.walizaliwa watano yeye ni watatu kati ya wanaume wawili, na wasichana watatu, wakwanza ni kaka yao.alipita akamsalimia baba yake, na kupitiliza chumbani. Hakika alijikuta anawaza sana matukio, yaliyomtokea shule. " mmh!! Au vicent amepata msichana mwengine?". Alijiuliza."kama ni kweli sitakubalii kwanza sina imani hiyo, labda atakuwa na jambo lingine, ila shule ile nzima, hakuna anaenikamata kwa uzuri".alijiwazia mwenyewe,akijiuliza na kujipa majibu mwenyewe. Ila gafla aka...... Itaendelea

Where do you want to donate?

Traktir Kopi
Bank BCA - An. Asep Saepul Anwar/ Rek - 648xxxx
Treat the creator to coffee by giving a small donation. click the arrow icon above

Chapisha Maoni

Copyright ©BongoLife - All rights reserved.

Redesign by bloggun.xyz
Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
More Details