MOYO ULIOJAA MAUMIVU SEHEMU YA 40

MOYO ULIOJAA MAUMIVU

SEHEMU YA 40

Kuhusu suala la ugonjwa wa Rachel, Theo hakutaka kumwambia mke wake, alijua kabisa angemchanganya zaidi hivyo aliamua kutulia kwa kubaki kimya mpaka pale ambapo tatizo hilo lingeanza kujitokeza.
Nyumbani, Violeth hakuwa na furaha, moyo wake ulimuuma mno, kila alipokuwa akimwangalia mtoto wake huyo alihisi maumivu makali, wakati mwingine alimlaumu Mungu kwa kumchukua mtoto wake ambaye alikuwa na mipango naye mingi lakini kuna kipindi alimuomba msamaha kwa kuwa kile kilichotokea, kilipangwa hata kabla ya yeye kuzaliwa.
Siku ziliendelea kwenda mbele, baada ya mwezi mmoja, Theo akarudi katika hali ya kawaida na kuendelea kufanya kazi zake za muziki. Alirudi na nguvu mpya, alitoa nyimbo mbili ambazo aliamini zingefanya vizuri kabisa.
Alichokitegemea ndicho kilichotokea, zilikuwa nyimbo kali sana ambazo zilipendwa na kila rika, kila mtu aliyezisikia aligundua kabisa kwamba Theo alirudi kivingine, alirudi na nguvu mpya ya kufanya ngoma kali zaidi.
Alichokifanya ni kufanya video zake, hakuzifanyia nchini Tanzania, aliamua kusafiri na kuelekea nchini Afrika Kusini na kuzifanyia huko. Kila mtu aliyeziona video hizo baada ya kuachiwa alichanganyikiwa, zilikuwa kali na zilizomfanya kuonekana kuwa mwanamuziki mwenye jina kubwa, hatari na aliyeiwakilisha vizuri Tanzania.
Alipokuwa huko, hakuacha kuwasiliana na mke wake, kila siku ilikuwa ni lazima kuzungumza naye kupitia video. Alimuona mtoto wake, alimsalimia, moyo wake ulikuwa na furaha mno kuiona familia yake ikiwa salama lakini kila alipokumbuka kwamba Rachel alikuwa na tatizo kwenye moyo wake, aliumia mno.
“Mbona umebadilika ghafla?’ aliuliza Violeth huku akimwangalia mume wake kwenye kompyuta yake kupitia mtandao wa Skype.
“Hapana! Nipo kawaida.”
“Kweli?”
“Yeah! Nipo kawaida. Nikuletee zawadi gani mpenzi?” aliuliza Theo, alijitahidi kumtoa mke wake katika suala la kutokuwa na furaha.
“Yoyote tu mpenzi!”
“Basi sawa, nitakufanyia sapraizi moja kubwa mno!”
“Kweli?”
“Niamini mpenzi!”
“Nakupenda sana!”
“Nakupenda pia.”

Where do you want to donate?

Traktir Kopi
Bank BCA - An. Asep Saepul Anwar/ Rek - 648xxxx
Treat the creator to coffee by giving a small donation. click the arrow icon above

Chapisha Maoni

Copyright ©BongoLife - All rights reserved.

Redesign by bloggun.xyz
Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
More Details