WANAWAKE TUKIOLEWA TUUNGANISHE FAMILIA NA TUSIWE WABOMOAJI

➿➿➿➿➿➿➿➿➿➿

*Kwenu wadada*

**

*-------•<°○●●○°>•-------*

Naomba niwausie wanawake  ambao, wameolewa na kwa wale wanaotarajia kuolewa
 namna ya kujenga na kuunganisha familia yako.

Mwanamke unapoolewa kumbuka unaenda kwa familia nyingine mpya, yenye baba, mama, kaka na ndugu wa mumeo.


Wewe ndio huwa kiungo muhimu na mhimili wa aidha umfanye mumeo apende au asielewane na ndugu zake kabisa kwa namna wewe utakavyoishi nae, katika kumjenga na kumshauri .

Tukumbuke  hakuna kitu kizuri kama heshimu. Onyesha heshima kwa kila mtu katika ndoa yako kwa kujistiri na kauli nzuri kwa watu wote, jenga mazingira ya kupenda wasijute kwako kuingia katika familia yao.

Kuna wanawake wachoyo jamani anamnyima ndugu wa mume chakula ambacho kijana wao amekitafuta sio vizuri tujifunze kuacha uchoyo.

Roho mbaya! Kuna baadhi ya wanawake wana roho chafu kiasi cha kuwa hataki mume asaidie kwao hata kidogo. Huu ni ubakhili wa hali ya juu na Allah mtukufu anachukia watu mabakhili.


kuna baadhi yetu tuna tabia ya kununa familia ya mume wajapo majumbani kwetu kututembelea, hii ni tabia mbaya, badilikeni

Tabia ya Kunyanyasa na kuchongea watoto wa mumeo  kama ulimkuta alizaa kabla au ndugu zake mume kwa lengo la kuhamisha upendo kwa kaka yao, tuache, watendee wema watoto wa mwenzia kama vile wewe ungependa wako atendewe kwani maisha ni mzunguko na Allah ndie mpangali na mlipaji.

Mwanamke akiwa na hekma na busara atakuwa mlezi na kiunganishi ila akiwa jeuri na kibri atakua mbomoaji.

Usimfanye mumeo ajute kukuoa dada, mfanye mumeo ajute kuchelewa kukufahamu mapema.

Subra kwa ndugu wa mume kwa sababu mara nyingi nao huwa na matatizo yao na balaa, vichuki bila sababu, hapa subra itatakikana na hali ya juu.


*Ya Rabi! tupe subra  na upendo wanawake wote!*

*------•<°○●●○°>•------*

```Ukiyapenda yachukue kama yalivyo```

➿➿➿➿➿➿➿➿➿➿
Where do you want to donate?

Traktir Kopi
Bank BCA - An. Asep Saepul Anwar/ Rek - 648xxxx
Treat the creator to coffee by giving a small donation. click the arrow icon above

Chapisha Maoni

Copyright ©BongoLife - All rights reserved.

Redesign by bloggun.xyz
Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
More Details