MOYO ULIOJAA MAUMIVU SEHEMU YA 39

MOYO ULIOJAA MAUMIVU

SEHEMU YA 39

Aliumia moyoni mwake, kile alichoambiwa hakutakiwa kukisikia kabisa, alikumbuka jinsi alivyoishi na mume wake, walivyokuwa na mipango mingi kuhusu watoto wao, walipanga mambo mengi, waliwafanyia shopping, waliwanunulia kila kitu mpaka kuwaandalia majina lakini mwisho wa siku, kila kitu kilionekana kwenda hovyo.
Theo ndiye alikuwa mfariji wake pekee, alilia sana lakini mwanaume huyo alikuwa pembeni yake na kuanza kumbembeleza kwa maneno mengi ya kutia moyo, maneno ambayo aliamini yangeweza kumsahaulisha mke wake juu ya watoto wake hao.
“Violeth! Usilie, hutakiwi kumkufuru Mungu. Kumbuka kila kitu kinachotokea ni mipango ya Mungu, kulia sana inamaanisha kwamba unakosoa kazi zake alizozifanya. Nyamaza, kama amemchukua mtoto wetu mmoja, ametuachia mmoja kwa sababu zake, naomba umshukuru Mungu kwa kila jambo,” alisema Theo kwa sauti ya chini, karibu kabisa na sikio la mke wake.
“Ninaumia sana...moyo wangu unaumaaaa....” alisema Violeth.
“Najua! Nimeumia pia kama wewe unavyoumia ila kuumia kwangu, machozi yangu hayawezi kumrudisha Harry! Naomba unyamaze mpenzi....” alisema Theo huku akimbembeleza mke wake huyo.
Mwisho wa siku Violeth alitakiwa kukubaliana na ukweli wa kile kilichotokea, kwamba mtoto wake mmoja alifariki dunia na kubaki mmoja.
Waliendelea kufarijiana mpaka pale walipokabidhiwa mwili wa mtoto wao na kwenda kuuzika katika makaburi yaliyokuwa nyuma ya hospitali hiyo.
Stori kuhusu kile kilichotokea zikaanza kusambaa kila kona, watu waliwaonea huruma, kila mmoja alisikitika mno kwani walikumbuka namna mwanamke huyo na mume wake walivyokuwa wakiwaambia kuhusu mapacha hao, jinsi watakavyotokea kuwapenda na kuwalea katika malezi mazuri lakini mwisho wa siku hawakufanikiwa kuwa na watoto wote wawili.
Watu wakawatumia salamu za pole, waliguswa na wengine kwenda kuwatembelea nyumbani kwao. Kwenye mitandao ya kijamii, ni stori kuhusu familia hiyo tu, ndiyo walikuwa watu maarufu kuliko mastaa wote nchini Tanzania hivyo hata viongozi wa serikalini na watu wengine wote waliwapa pole kwa kile kilichokuwa kimetokea.

Where do you want to donate?

Traktir Kopi
Bank BCA - An. Asep Saepul Anwar/ Rek - 648xxxx
Treat the creator to coffee by giving a small donation. click the arrow icon above

Maoni 1

  1. Mpenzi wangu aliachana na mimi, najua ilikuwa kosa langu ambalo lilimfanya aachane na mimi, akanipata nikiongea juu yake, kuna kijana niliyemwita rafiki yangu alinivuta na kufanya naye mapenzi kisha mpenzi wangu akatushika, basi aliachana na mimi, ninampenda sana, nilifurahisha kwa wiki na miezi hakukubali kunikubali, nilikuwa nikisoma mkondoni jinsi ya kumrudisha mpenzi wangu basi nilikuta na makala juu ya jinsi mwanamke alirudi Mumewe aliyempa talaka, alisema kuwa Dk Lomi amsaidia alifanya sala kadhaa na mumewe amerejea kwake, basi na mimi nikawasiliana na Dr Lomi na kuelezea kile kilichotokea kisha akanisaidia kufanya maombi kadhaa na mpenzi wangu akarudi akiniombea alijuta kuwa bado ananipenda na leo tumerudi pamoja na naahidi kamwe hatutazungumza juu yake na leo tunafurahi, ikiwa unahitaji pia Msaidizi wa Dk Lomi kuwasiliana naye kwenye Line ya nambari ya WhatsApp; +2349034287285 unaweza pia kumtumia barua pepe; [email protected] kwa msaada

Copyright ©BongoLife - All rights reserved.

Redesign by bloggun.xyz
Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
More Details