UNATAKA KUITEKA AKILI YAKE BASI MUAMBIE UNAVYOJISIKIA!

UNATAKA KUITEKA AKILI YAKE BASI MUAMBIE UNAVYOJISIKIA!

Mara nyingi wanaume ni watu wa vitendo zaidi kuliko maneno, lakini wanasahau kua wanawake hupenda maneno zaidi na wakati mwingine hata kama vitendo ni vizuri lakini wanawake hukumbuka maneno matamu ambayo huambiwa na wapenzi wao, kwa maana hiyo mara kwa mara hembu penda kumuambia mke/mpenzi wako kuwa unampenda na unamjali, mfanye ajihisi kuwa bado ni muhimu kwako.

Kwa mfano, kwa mwanaume kumhudumia mke/mpenzi wake wakati anaumwa ni jambo la upendo, kumpa pesa kwajaili ya matibabu inamaana zaidi kuliko hata kumuambia pole, lakini katika akili ya mwanamke haya ni amjukumu na si upendo, mwanamke ni ngumu sana kukumbuka hiki kitu lakini ni rahisi kukumbuka pole ambayo ulimuambia, namna ulivyomuuliza anavyojisikia na namna ulivyomuambia “Nakupenda sana, unavyoumwa najisikia na mimi kama kuumwa!”

Atakumbuka meseji uliyomuandikia wakati uko ofisini na kumuuliza “Unajisikiaje sweetee missing u, umekula kweli wewe?” ni ngumu sana kwa mwanamke kumsahau mwanaume ambaye anajua namna ya kucheza na maneno yake, kujua nini chakumuambia anapokua na mawazo, anapokua kagombana na mashoga zake, anapokua hajisikii vizuri, anapofiwa na wakati mwingine wowote ule anapohitaji faraja ya namna falani kama mwanaume unatakiwa kuwepo.

Huwezi amini lakini malalamiko mengi ya wanawake hutokana na kukosekana kwa mawasiliano, mwanamke anaweza kuvumilia mwanaume ambaye hamhudumii kwa chochote, tena wengi hasa katika mahusiano ya kawaida hata hawahudumiwi, lakini mwanaume akikaa siku mbili tatu hajapiga hata simu au kutuma meseji mwanamke huanza kujihisi kama vile kaachwa. Hivyo hata kama pesa unatuma lakini kama hakuna mawasiliano basi jua mwanamke wako hahisi upendo wa aina yoyopte ile. Trust me  lv all people

Where do you want to donate?

Traktir Kopi
Bank BCA - An. Asep Saepul Anwar/ Rek - 648xxxx
Treat the creator to coffee by giving a small donation. click the arrow icon above

Chapisha Maoni

Copyright ©BongoLife - All rights reserved.

Redesign by bloggun.xyz
Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
More Details