KWANINI MABINTI WENGI HAWAOLEWI?

SABABU ZA WASICHANA WENGI   KUTOOLEWA
KWANINI MABINTI WENGI HAWAOLEWI?

*zifuatazo ni baadhi ya sababu kwanini mabinti wengi wanashindwa KUOLEWA..*

*1.VIGEZO VISIVYO NA MSINGI.*
*Kuweka vigezo vingi na kuchagua chagua sana inaweza ikawa ni sababu ya kufanya mabinti wengi wasiolewe.*

*Binti unakuta anataka mwanaume awe amesoma, mrefu, handsome, sijui awe na kazi nzur, awe na upendo wa kweli, na mambo mengi kama hayo.*

*Wanaume wanaokidhi vigezo hivyo ni wachache sana na kimsingi inawezekana wasiwepo kabisa. Mwisho hujikuta umri unaenda bila ya kuolewa au kuangukia kwenye mikono ya Wanaume ambao ni matapeli wa mapenzi.*

*kuna msemo usemao, "ndege mjanja hunasa kwenye tundu bovu" na mwingine ufananao na huo unaosema "mchagua nazi hupata koloma".*

*2.NAMNA UNAVYOJIWEKA.*
*Jinsi unavyojiweka ndivyo watu watakavyokuchukulia. Mavazi unayovaa, marafiki ulionao na hata tabia yako kwa ujumla.*

*Mabinti wengi wanafeli sana kwenye eneo la mavazi, mavazi ya kuacha maungio ya ndani wazi yanawashushia heshima mabinti wengi sana bila wao kujua, wengi wanaona kama wanaenda na wakati lakini wanajidhalilisha.*

*Hakuna mwanaume anayependa kuoa mwanamke asiyejiheshimu, kama yupo basi hatakuwa muaoji. Mwanaume gani anayependa kutembea na mkewe akiwa maziwa yapo wazi yananing'inia kama yanataka kuanguka?*Sketi fupi mapaja yote yapo wazi na tena ina mpasuo?* *Suruali imembana mpaka maumbile ya ndani, michirizi ya nguo ya ndani inaonekana*

*Sidhani kama kuna mwanaume anayependa mwanamke ambaye mwili wake ni maonyesho ya saba saba, Sidhani kama kuna mwanaume anayependa kuwa na mwanamke ambaye hata nyumbani kwao hana ujasiri wa kumpeleka, Sidhani kama kuna mwanaume anayependa kuwa na mwanamke ambaye starehe yake ya usiku na Mali yake ipo wazi kwa marafiki zake na watu kama Mali ya umma.*

*Niwasaidie dada zangu,ukivaa mavazi ya ajabu ajabu utavutia Wanaume wa kulala na wewe na kukuacha na si waoaji, utakuwa ni kiburudisho cha usiku mmoja na si mwanamke wa maisha.*

*3.MANENO UNAYOJITAMKIA.*
*Vijana wengi wamekuwa na desturi ya kujisemea maneno ya laana bila kujua yana madhara gani katika maisha yao.*

*Utakuta Binti kwa sababu aliumizwa na kijana fulani basi, anasema Wanaume wote ni wale wale, sijui siku hizi Hakuna waoji, mara Wanaume wote ni waongo, baba mmoja na mama mmoja.*

*Sikia nikuambie, kinywa chako kina uwezo wa kuumba.* *Kila neno baya au zuri unalojitamkia ndivyo litakuwa kwako.*

*Kama Unasema Wanaume wote ni waongo basi usishangae Kila mwanaume atakayekuja kwako akiwa muongo.* *Kama Unasema sina shida ya kuolewa basi miaka 30 itakukuta ukiwa nyumbani kwa baba yako. Chunga kinywa Chako.*

*4.KUTOKUSHUKA.*
*Utii ni tatizo kwa mabinti wengi sana wa sasa. Wengi hawakubali kushuka, hawataki Kuongozwa wanataka kujiongoza wenyewe.*

*Kumtii mwanaume wanaona kama ni jambo la kizamani, wanaita mfumo dume hivyo wanataka kuishi katika mfumo Jike.*

*Napenda kusema wasichana wengi vazi la Suruali limeathiri mpaka fikra zao, hata akili zao pia zimevaa Suruali.*

*Binti Hakuna mwanaume anayependa kuwa na mwanamke ambaye si msikivu (jike dume), kama hautaki Kuongozwa basi wewe ni mwanaume sasa unataka mwanaume wa nini?*

*Binti kaa kwenye nafasi yako. Jivike kiremba cha Hekima na Utii.*

*5.MAAGANO ULIYOWEKA HUKO NYUMA.*
*Kama kuna mtu mliahidiana kuwa mtaona halafu kwa sababu zisizo na msingi ukamuacha, basi hii inaweza ikawa ni moja ya sababu ya kukufungia baraka yako ya ndoa.*

*Kama kuna mtu ana nung'unika kwa ajili yako, kama kuna mtu analia kwa ajili yako huu unaweza ukawa mwiba kwako usiifikie ndoa au ukaifikia lakini isiwe salama.*

*Kama kuna watu ulishindwa kutimiza ahadi uliyowaahidi basi huwo nimkosi kwako*

Binti.

*jitambue*

Where do you want to donate?

Traktir Kopi
Bank BCA - An. Asep Saepul Anwar/ Rek - 648xxxx
Treat the creator to coffee by giving a small donation. click the arrow icon above

Chapisha Maoni

Copyright ©BongoLife - All rights reserved.

Redesign by bloggun.xyz
Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
More Details