UTAPELI MPYA WA FEDHA .

UTAPELI MPYA WA FEDHA .

 SAMBAZA UJUMBE UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI

Tapeli huyu anaitwa JOSEPH MGAWE

Habari ndugu Watanzania wenzangu popote mlipo nawasalimu sana. Nawapa tahadhari kubwa kuhusu utapeli mpya ambao unaendelea kufanywa na baadhi ya matapeli hapa nchini na umeumiza watu wengi na kuleta mfarakano mkubwa sana kati ya marafiki na ndugu .

Kuna mtandao hatari wa watu wanajifanya wana uwezo wa kutengeneza pesa na kuzizalisha kwa kutumia madawa na karatasi maalum.

Wanachofanya ni kukuaminisha na kukuonyesha mfano wanavyotengeneza hizo pesa na kuzizalisha Mara 3 , mfano ukiwa na laki moja zitazalishwa inakuwa laki 3 . ukiwa na laki 2 zitazalishwa inakuwa laki 6 , ukiwa na Milioni moja zitazalishwa na kuwa Milioni 3 .

WANACHOFANYA: Anakuwa na karatasi za rangi ugoro  zilizokatwa size ya noti ya elfu kumi , hizo karatasi anazipanga pamoja na fedha halali Kila noti ya elfu 10 inabeba karatasi mbili , akimaliza kuzipanga anazifungia kwenye karatasi ya Rambo alafu anachukua dawa kwenye kichupa kidogo ananyonya na sindano alafu anazidunga zile pesa huku akiwa amevaa Gloves , baada ya dakika 10 zile fedha atazitumbukiza kwenye Jag la umeme lenye maji na kuchemsha maji huku akimimina dawa , baadae atazitoa zikiwa ni elfu kumi mpya zote ikiwa ni fedha halali na zile karatasi alizopanga zimekuwa pesa .kama ulitoa laki moja inakuwa laki 3 anakuachia zote au anakuambia nipe laki moja wewe chukua laki mbili .

Hapo ataondoka na kukuambia ukiwa na mzigo mkubwa unapata faida kubwa zaidi , atakuachia namba zake za  simu .  anatembea na chupa yake ikiwa na dawa ya kemikali imeandikwa kabisa dawa hii ni kutengenezea kuanzia mzigo wa Laki Tisa , milioni 5 , Milioni 10, Milioni 7, Milioni 20  na Milioni 30 anapima na uwezo wako wa kifedha .

Sasa akikuonjesha utamu  na wewe utahangaika kutafuta fedha ili uzalishe , au utawaambia ndugu na rafiki zako na huyo tapeli yuko tayari kwenda kwa hao rafiki zako kuonyesha mfano wa anavyozalisha pesa tena anakuja nyumbani kwako sebuleni kabisaa au chumbani au Hotelini.

Akishawaroga hivo mtaweweseka kutafuta pesa nyingi zaidi , mtamuita njoo tutengenezee tuna mzigo mkubwa wa milioni kadhaa , atazuga yupo bize anafanya kazi sehemu , na kweli wako bize kusafiri huku na kule , anakwambia andaa mzigo tayari wa noti za elfu kumi kumi , akija nyumbani kwako kama kawaida mtazipanga pesa zoote kwa kubebanisha na karatasi kama alivyoonyesha mfano awali , atazifunga kwenye mfuko wa rambo na kuzibana na solatepu mkiwa wote hapo afu anaziwekea dawa kwa kutumia bomba la sindano , atakwambia mziache kwa dakika 30 ili mje mzitoe mzisafishe .

ATAZUA JAMBO : Baada ya kufanya hivyo atazusha jambo mfano dawa hii imeganda inahitaji kidonge ili ije isafishe pesa vizuri au atakwambia inahitajika sabuni ya AERIAL au OMO au atazusha hoja nyingine kulingana na mazingira ya nyumbani kwako , atauliza lilipo duka la madawa ili anunue kidonge au duka akanunue sabuni ya OMO, ataacha Kila kitu hapo , akitoka hapo ndo kimojaa hutamuona tena. Anakuachia hizo pesa zimefungwa kwenye Rambo ukidhani pesa. Ukimpigia simu ataleta sababu kibao Mara hili kidonge hakipo duka la madawa mpaka hospitali ya Wilaya au Mkoa , atakuhakikishia mzigo uko salama na utaharibika ndani ya siku 21 . danadana zitakuwa nyingi na atakutisha ukiufungua huo mzigo pesa zako zitaharibika .

UMEULA WA CHUYA NDUGU HAPO UMEACHIWA KARATASI NA PESA ZAKO ZOTE  ZIMECHUKULIWA .

Watu wengi wametapeliwa na kubaki masikini , Dada yangu katapeliwa Milioni 5 na rafiki wa Dada kapigwa Milioni 10 , na kaka mmoja nae kapigwa milioni 20 , Mwalimu mmoja yeye alienda kukopa bank Milioni 8 nazo zimeliwa . wamebaki kulia na kusaga meno .

Ninavyoandika hapa Dada yangu kafukuzwa na mumewe kwasababu alichukua fedha za dukani na zimepotea .

Baada ya kuchunguza kwa makini imeonekana Vijana hao matapeli wana tokea Sumbawanga , Mbeya Mjini , Chunya ,  na Iringa na wanatumia kiinimacho cha uchawi.  Wakifanya utapeli wanakimbilia Mbeya na Sumbawanga .

Sambaza ujumbe huu kwenye MAGROUP yote na mitandao ya Kijamii ili kuokoa wengine wasitapeliwe maana mtandao huu wa utapeli ni mkubwa sana .

Angalieni picha zao tumezikuta kwenye simu aliyeisahau mmoja wao Baada ya kutokomea .

Je umewahi kutapeliwa kwa mtindo huu ?  Wakija kwako wakamate haraka na kuwafikisha Polisi maana tumewaripoti Polisi Central Dodoma .

By Zakia , Dodoma.

Where do you want to donate?

Traktir Kopi
Bank BCA - An. Asep Saepul Anwar/ Rek - 648xxxx
Treat the creator to coffee by giving a small donation. click the arrow icon above

Chapisha Maoni

Copyright ©BongoLife - All rights reserved.

Redesign by bloggun.xyz
Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
More Details