Jinsi ya kutunza nywele zako | Natural hair

kuna vitu vingi vinavyoweza kufanya nywele zako zikakosa afya na mvuto, vitu kama vumbi, upepo, mvua, jua, maji na madawa tunayoweka kwenye nywele zetu pamoja na vyakula tunavyokula ni chanzo kikuu cha nywele zetu kuharibika na kukosa afya na mvuto. leo nimekuletea vidokezo vichache vya jinsi ya kutunza nywele zako.
kuna vitu vingi vinavyoweza kufanya nywele zako zikakosa afya na mvuto, vitu kama vumbi, upepo, mvua, jua, maji na madawa tunayoweka kwenye nywele zetu pamoja na vyakula tunavyokula ni chanzo kikuu cha nywele zetu kuharibika na kukosa afya na mvuto.
leo nimekuletea vidokezo vichache vya jinsi ya kutunza nywele zako.

Jinsi ya kutunza Natural hair

1.kata ncha za nywele zako


kukata ncha za nywele zako kunasaidia kufanya nywele zako kujizaa upya, mara nyingi seli katika ncha za nywele hufa. seli zinapokufa huzui nywele zinazozaliwa kushindwa kustawi vyema na hivyo kuzifanya nywele zako kukosa afya. japo wanawake wengi huwa hawapendi kukata ncha za nywele zao wakihofia nywele zao kuonekana fupi. lakini ukweli ni kwamba unapokata ncha za nywele zako unasaidia nywele zako kupata nafasi ya kukua vizuri na kuwa zenye afya nzuri na kuvutia.

2.onya nywele zako angalau mara moja kwa wiki


kuonya nywele zako angalau mara moja kwa wiki kutasaidia kuzifanya nywele zako ziwe na afya. hata kama uko busy sana basi jitahidi isipite wiki mbili bila kuonsha nywele zako.

3.tumia shampoo inayoendana na nywele zako


tumia shampoo inayoendana na nywele zako, kuna nywele za aina tofauti. kuna nywele kavu, zenye mafuta, mchanganyiko, na pia kuna nywele nyepesi, laini, ngumu na nzito. zipo aina tofauti za shampoo zinazoendana na aina ya nywele zilizopo . hivyo basi ni vyema unapotaka kuosha nywele ukajua ni aina gani ya shampoo utumie, pia kwenye condition napo unatakiwa kufanya hivyo hivyo.


4.Zipe nywele nafasi


nywele nazo huitaji nafasi,kuchana nywele kila siku,  kuzipaka nywele jelly kila siku, kuzichana mitindo tofauti, kuziwekea gundi na mafuta tofauti tofauti huzifanya nywele zako zichoke na kukosa afya. hivyo unatakiwa mara moja moja unazipa nywele zako nafasi ya kumupumzika. zipumzishe nywele zako kwa kusuka mtindo ya kawaida au rasta za mabutu. ​

5.usichane nywele kwa nguvu zikiwa mbichi.


jaribu kuzichana nywele kwa kichanuo kikubwa, au jaribu kuziacha mpaka zikauke ndo uzichane. unapochana nywele mbichi tumia kitana kikubwa na chana taratibub ukianzia nyuma kuja mbele. kuchan nywele zikiwa mbichi bila kufuata utaratibu kutafanya nywele zako zikatike na ziharibike.

6.zilinde nywele zako unapokuwa unaogelea


unapokuwa unaogelea baharini au kwenye bwawa la kuogelea, jaribu kuzifunika nywele zako au zipake mafuta ya kuzui zisiharibike na maji, na unapotoka kuogelea zisafishe nywele zako kwa maji safi na uzikaushe.

7.kula vyakula venye protin na matunda


kula vyakula venye protin na matunda kutasaidia kuimalisha afya ya nywele zako na kuzifanya ziwe nzuri na za kuvutia.

8.Zifunge nywele zako kabla ya kulala


unapotaka kulala hakikisha unazifunga nywele zako, unaweza kuzisuka mabutu au kuzifuna vizuri na kuzibana. kulala huki ukiwa umeziachia nywele zako hufanya nywele zikatike na kuharibika.

9.Tumia mafuta asili


badala ya kutumia mafuta yenye kemikali nyingi kutoka viwandani, jaribu kutumia mafuta ya asili katika kutunza nywele zako. tumia mafuta kama ya nazi au parachichi kupaka nywele zako.

10.zilinde nywele zako na jua


wakati utakapokuwa unaelekea kwenye sehemu yenye jua kali, vumbi au upepo. zilinde nywele zako kwa kuzifunika na kofia, scarf au mtandio.

 Steaming ya nywele za asili | Natural hair product

Mahitaji;
-parachichi
-yai la kuku Wa kienyeji
-Asali

hatua:
i) chukua parachichi lako likate toa ile nyama ya ndani weka kwenye chombo ili utengeneze mchanganyiko wako
ii) chukua yai lako pasua chukua kiini tu cha yai lako changanya na parachichi
iii) chukua asali yako pima vijiko viwili au vitatu vikubwa changanya kwenye ule mchanganyiko koroga Hadi vyote vichanganyike vizuri
Baada ya hapo osha nywele zako pakaa huo mchanganyiko na ukae kwenye steamer mda kadhaa
na baadae uzioshe hapo utakuwa umeboresha nywele zako kiasili zaidi


Kuza nywele kwa haraka | Natural hair


Kila baada ya siku nne uwe na utaratibu wa kupakaa mchanganyiko wa hina na mayai, iwe na paste nzito kiasi, upake katika mizizi ya nywele, ukimaliza kupaka nywele zifunike kwa mfuko maalum ili zipate joto kwa muda wa masaa mawili,


Baada ya hapo zioshe kwa maji na shampoo, lakini maji yawe ya baridi yasiwe ya motooo au vuguvugu, yani yawe maji ya kawaida. Baada ya kuziosha zikaushe kwa taulo


NB: Nywele hazichanwi zikiwa na maji zimerowa kwani zitasababisha kung'oka kwa nywele na kusababisha upunguf wa nywele. Nywele zikishakauka. Paka mafuta ya nazi, au your favourate muhimu upake katika mizizi ya kichwa.


Na wakati unapaka mafuta kichwani kichwa kiinamishe chini, kiangalie chini ndio upake mafuta kichwa chako husaidia msukumo wa damu kufikia katika kichwa vizuri na kupata stimulation kwa kutumia ncha za vidole huku ukifanya massage kichwa taratibu kwa mda wa dakika tano, ukimaliza anza kuzichana taratibuu mpaka zilainike na uzibane.


Jaribu kwa siku uchane nywele mara mbili asbuh na jion, na nywele muda wote ziwe zenye mafuta. jizoeshe kufanyia massage kichwa chako kila wakati unaopaka mafuta kichwani.
Uhai wa nywele ni mafuta kama ilivyo uhai wa binadamu utakuepo iwapo kuna maji.

TIBA YA NYWELE ZINAZO KATIKA KWA KUTUMIA KITUNGUU MAJI

Kitunguu maji kina sulphur ambayo husaidia kutengeneza tishu za collagen katika mwili ambapo collagen husaidia kunurisha nywele na ngozi. Hivyo tunaweza kusema kuwa kitunguu maji husaidia kukuza nywele na kwa wale wenye nywele za kukatika, kupaka kitunguu maji mara kwa mara kinaweza kusaidia kupambana na tatizo hilo.

Je utatumiaje kitunguu ili ufaidike na kitunguu maji kwa nywele zako. Soma zaidi hapa chini.

Jinsi ya kuandaa

Chukua kitunguu kimoja au viwili kutegemeana na ukubwa wa kitunguu chenyewe. Fuata hatua zifuatazo:
Osha vizuri kitunguu au vitunguu na kisha ukimenye au uvimenye
Kata kitunguu au vitunguu vipande vidogo vidogo ili iwe rahisi kusaga au kutwanga
Saga kwenye brenda au twanga kwenye kinu , njia yoyote ile ambayo kwako ni rahisi kwako. Visage au vitwange mpaka vilainike kabisa ili uweze kutoa maji kwa urahisi.
Ukishasaga au kutangwa vitunguu , vichuje vizuri ili upate maji maji .Zingatia usiweke maji kwa hivi vitunguu.

Jinsi ya kupaka

Nywele sio lazima ziwe safi maana unapaswa kuziosha baada ya kupaka maji ya vitunguu.
Chukua pamba ambayo utatumia kupaka hayo maji ya vitunguu kwenye nywele zako. Paka zile sehemu ambazo nywele zimekatika. Unaweza pia paka kichwa kizima.
Baada ya kupaka unapaswa kuvaa kofia ya plastic na kitambaa kwa juu ili kuweza kupata joto . Tahadhali usikae kwenye mashine ya steam au dryer.
Ukiwa na kofia ya plastic na kitambaa kwa juu ya nywele zako , ukae hivyo hivyo kwa masaa manne hadi matano.
Baada ya hapo unaweza kuosha na kukausha nywele zako na kuweka style yoyote ile.
Hitimisho
Ni vema kufanya zoezi hili la kupaka vitunguu walau mara mbili kwa mwezi. Ikiwa harufu ya kitunguu ni kali, unaweza weka asali kidogo kwenye maji ya vitunguu.
Kwa matokeo mazuri ya kukuza na kutunza nywele zako tumia vitunguu vidogo kufanya zoezi nililoeleza hapo juu.


Where do you want to donate?

Traktir Kopi
Bank BCA - An. Asep Saepul Anwar/ Rek - 648xxxx
Treat the creator to coffee by giving a small donation. click the arrow icon above

Copyright ©BongoLife - All rights reserved.

Redesign by bloggun.xyz
Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
More Details